LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 11, 2024

MAUMIVU: TYR AGAIN AACHIA NGAZI UWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI SIMBA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Soka ya Simba Salim Abdallah Muhene maarufu 'Try again', ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, leo.


Try Again ametangaza uamuzi huo kufuatia

shinikizo kubwa kutoka kwa wapenzi na wanachama wa Simba Sc.


“Nimechukua uamuzi huu kwa manufaa mapana ya klabu ya Simba” amesema Try Again, lakini akasisitiza kuwa ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Simba.


Try Again aliteuliwa kushika wadhifa huo na Mwekezaji wa Simba SC, Mohammed Dewji (Mo) Septemba 29, 2021.


Tangu aingie madarakani Klabu hiyo imekuwa haina matokeo ya kuridhisha hivyo kusababisha kuwepo kwa shinikizo la kutaka viongozi wa juu wa klabu hiyo kuachia ngazi.

Try Again

Sorce: https://www.instagram.com/p/C8FGUpoi0cy/?igsh=MWkzdHgwM3g0MHBnbQ

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages