Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayehusika na Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo wakionesha kwa waandishi wa habari kitabu cha taarifa ya hali ya dawa za kulevya wakati wa mkutano katika ukumbi wa habari bungeni Dodoma Mei 16, 2024.
Mhagama akisisitiza jambo.
Baadhi ya wanahabari wakiwa kazini.
Kiasi cha Tani 1.757.56 za dawa za kulevya aina ya bangi kilikamatwa kwa mwaka 2023 kikihusisha watuhumiwa 8,803 kati yao wanaume 8,180 na wanawake 623.
Hiyo sehemu ya taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayehusika na Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama mbele ya vyombo vya habari jijini Dodoma Mei 16, 2024,alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2023.
Pia ameeleza kuwa katika kipindi hiki kumeibuka uingizaji na matumizi ya bangi mpya inayoitwa skanka ambayo inadhaniwa kuwa inazalishwa katika Nchi za Kusini mwa Afrika.
Skanka ni mchanganyiko wa aina mbili za bangi, cannabis sativa na cannabis indika ikiwa na kiasi kikubwa cha THC hivyo kuwa na athari kubwa kwa watumiaji.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇