LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 16, 2024

TAIFA GAS WAUNGA MKONO KAMPENI YA RAIS DK. SAMIA, WAGAWA BURE MITUNGI 300 HANDENI MJINI, LEO

Handeni, Tanga
Kampuni yaTaifa Gas imegawa bure mitungi 300 iliyojazwa gesi kwa wakazi mbalimbali wa Handeni Mjini kuunga mkono kampeni ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ya kumtua mzigo wa kuni mwanamke na kutunza mazingra kwa kutumia nishati safi ya kupikia.
 
Akikabidhi mitungi hiyo leo Mei 16, 2024, kwa wakazi wa Handeni Mjini, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando, aliishukuru Kampuniya hiyo kwa kuanza na Handeni kutekeleza kampeni hiyo na ndipo waende  sehemu zingine, na kuahidi kuwa Handeni watakuwa mabalozi wazuri wa Kamuni yaTaifa Gas.

Wakili Msando alisema Handeni ni kubwa na ina wakazi wengi, hivyo mitungi 300 haiwezi kutosha wakazi wote na badala yake alielekeza mitungi hiyo wapewe mabalozi ambao ni wawakilishi wa wananchi wakawe mabalozi wazuri kwa wananchi wao.

Miongoni mwa walionufaika na mitungi hiyo ya Taifa Gas ni pamoja na Madiwani wa kata zote za Handeni, Viongozi wa kidini, viongozi wa vyama vya siasa, MakatibuTarafa, Viongozi wa Serikali za mitaa, Vikundi vya Wajasiliamali na Vikundi vya Mamalishe.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Taifa Gas Angela Bhoke, akizungumza wakati wa hafla ya kugawa bure mitungi 300 ya kampuni hiyo kwa wakazi wa wilaya ya Handeni mjini mkoani Tanfa, leo Mei 16, 2024, ikiwa ni shehemu ya utekelezaji wa Kampeni maalumu ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama mzigo wa kuni na kuhifandhi mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando (mwenye vazi jeupe) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka la Taifa Gas Wilayani Handeni, wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya hiyo, leo
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando akizungumza baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Duka la Taifa Gas Wilayani Handeni, wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 300 ya Taifa Gas bure kwa wakazi wa wilaya hiyo, leo. Kisha Wakili Msando akagawa mitungi ya Taifa Gas kwa wananchi mbalimbali.👇
--------------------------------------------------------
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albart Msando akishangilia wakati akiwa na baadhi ya wananchi aliowagawia mitungi ya Taifa Gas.
Kinamama wanufaika wakiwa na mitungi yao ya Taifa Gas baada ya kukabidhiwa.
Mitungi ya Taifa Gas bwererere!

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages