LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 23, 2024

WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA MAONESHO YA KLINIKI ARDHI BUNGENI DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),  Hamad Abdallah kuhusu utendaji wa shirika hilo alipotembelea Maonesho ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  (Kliniki ya Ardhi) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Mei 23, 2024.

Dkt Aidan Kawinga akitoa maelezo kwa Waziri Mhagama jinsi ndege isiyo na rubani (Drone) inavyotumika kupima ardhi. Aliyevaa suti ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.

Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Global Survey, Daud Msungu akitoa maelezo kwa Waziri Mhagama kuhusu vifaa vyao vya kisasa vya kuchora ramani na kupima ardhi.
Waziri Mhagama akitembelea mabanda mengine yaliyoshiriki maonesho hayo yenye lengo la kuwajengea uelewa wabunge na wananchi kuhusu kazi mbalimbali za wizara hiyo.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203





 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages