LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 24, 2024

WATEULIWA 14 KUGOMBEA UBUNGE KWAHANI, ZANZIBAR, KAMPENZI KUANZA LEO

Na Mwandishi Maalum, Zanzibar

JUMLA ya wagombea 14 kutoka vyama vya siasa vyenye usajili kamili wameteuliwa kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Safia Iddi Muhammad leo tarehe 23 Mei, 2024 amesema Kati ya wagombea hao tisa ni wanawake na watano ni wanaume. 

Safia amesema wagombea hao wote ni wale waliojitokeza kuchukua fomu na kuzirejesha ndani ya muda uliopangwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Fomu za uteuzi kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo zilianza kutolewa kuanzia tarehe 17 hadi 23 Mei, 2024 ambayo pia ilikuwa siku ya uteuzi. 

Amesema uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi limekwenda vizuri na amevipongeza vyama vyote vilivyojitokeza kugombea nafasi hiyo.

"uteuzi wa wagombea katika Jimbo la Kwahani limekwenda vizuri  na tayari majina ya wagombea 14 waliojitokeza kuchukua fomu na kuzirejesha wameteuliwa kuwania kiti hicho," alisema  Safia.

Amewataja wagombea walioteuliwa na Vyama vyao katika Mabano kuwa ni   Bashir Yatabu Said (Demokrasia Makaini),  Nuru Abdulla Shamte (DP), Mwanakombo Hamad Hassan (NLD),  Zainab Maulid Abdallah (CCK), Tatu Omary Mungi (UPDP),  Khamis Yussuuf Mussa (CCM) na  Jarade Ased Khamis (AAFP).

Wengine ni  Kombo Ali Juma (NRA), Shara Amran Khamis (ADC), Naima Salum Hamad (UDP), Madina Mwalim Hamad (ADA TADEA), Amour Haji Ali (SAU), Mashavu Alawi Haji (UMD) na Abdi Khamis Ramadhan (CUF). 

Safia amesema tayari ameshakutana na wagombea wa Vyama vyote na wapo tayari kuanza kampeni.

Taarifa ya INEC iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Kailima, jijini Dodoma tarehe 02 Mei, 2024 kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo zitaanza tarehe 24 Mei, 2024 hadi tarehe 07 Juni, 2024 na uchaguzi utafanyika tarehe 08 Juni, 2024.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani,  Safia Iddi Muhammad akibandika fomu za uteuzi za wagombea 14 kutoka vyama vya siasa vyenye usajili kamili walioteuliwa kuwania nafasi ya kiti cha Ubunge Jimbo la Kwahani. Uteuzi w wagombea hao ulifanyika leo tarehe 23 Mei, 2024.
Baadhi ya wanachama na wagombea wa Vyama mbalimbali vya siasa vilivyosimamisha wagombea katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kwahani Mkoa wa Mjini Magharibi, Zazibar wakikagua fomu za uteuzi za wagombea zilizobandikwa leo baada ya uteuzi.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages