LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 25, 2024

MBUNGE ABOOD ATAKA WANAHABARI KUELEZA YANAYOFANYWA NA DKT.SAMIA

NA VICTOR MAKINDA, MOROGORO


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Dokta Abdulaziz Abood (pichani) amewataka waandishi wa habari mkoani Morogoro Kutumia kalamu zao vizuri kwa kuandika masuala mbalimbali yatakayo leta matokea chanya nchini.

Mhe. Mbunge amesema hayo wakati akihojiwa  na kituo  hiki kuhusu  mtazamo wake uhuru wa vyombo vya habari nchini. ambapo amesema wanahabari wananafasi kubwa Kuhamasisha masuala mbalimbali ya kimaendeleo  Ili kuunga serikali mkoano katika kuletea maendeleo wananchi.

Baadhi ya waaandishi wa habari wakiwa katika picha

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa kuwaletea maenendeleo wananchi Kwenye sekta ya afya , elimu,barabara  na maji lakini baadhi ya  watu wanabeza Utendaji kazi wake 

Amesema wanahabari Wana kila sababu ya kuhabarisha umma kuwaeleza  kila kinachofanyawa na Serikali  hasa katika kuwahudumia wananchi  Ili watu Wenye nia mbaya na serikali wasipate nafasi ya kusambaza uongo.


Amesema Jimbo la Morogoro limepokea fedha nyingi kutoka serikali kuu na kutekeleza miradi ya maendeleo hivyo tuna kila sababu ya kumshuru Dokta Samia  hususani  ujenzi miradi ya Maji .

Dokta Abood ameongeza Kwa kuse


ma serikali inathamini kazi nzuri inayofanywa na wanahabari katika kutangaza mafanikio ya serikali na kuibua  changamoto za Jamii Ili zitatuliww hivyo itaendelea kutoa ushirikiano katika Utendaji Kazi wao.

Mhe. Abood ni Mlezi  wa chama cha waandishi wa habari mkoa Morogoro (MORO PC) ambapo Leo yamefanyika maadhimisho ya siku  ya uhuru wa vyombo vya Habari kimkoa ambapo kitaifa yalifanyika Mei 3 jijini  Dodoma


Katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa chama Cha Waandishi wa Habari mkoa Morogoro Nikson Mkilanya amesema chama hicho kimeadhimisha kwa kupanda Miti mto lukulunge ambao unachangia Maji bwawa la mindu ambapo linategemewa kwa zaidi ya asilimi 70 upatikanaji huduma ya maji Kwa  wakazi wa mji wa Morogoro.


Amesema mabadiliko tabia nchi  yameleta athari kubwa nchini hivyo wanabari wanatakiwa kuunga mkono kwa vitendo  mapambano ya uharibifu wa vyanzo vya maji

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages