LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 19, 2024

ZIARA YA RAIS DK. SAMIA UTURUKI: MIKATABA MIWILI YASAINIWA KUHUSU ELIMU YA JUU, AZURU KABURI LA RAIS WA KWANZA WA NCHI HIYO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakishuhudia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Lela Muhamed Mussa na Rais wa Baraza la Utalii la Jamhuri ya Uturuki Abdullah Eren wakisaini hati za makubaliano kwa ajili ya kuanzisha ufadhili kwa wanafunzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Uturuki wanaohitimu katika Elimu ya Juu, jana, Aprili 18,  2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba na Rais wa Baraza la Elimu Profesa Uturuki Dk. Erol Ozvar wakitia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika Nyanja ya Elimu ya Juu baina ya Tanzania na Uturuki jana Aprili 18, 2024.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakiangalia album ya picha za matukio ya Ziara Rasmi aliyoifanya katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozwa kwenda kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal AtatĂĽrk katika makumbusho ya Anitkabir, AtatĂĽrk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima mbele ya kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal AtatĂĽrk katika makumbusho ya Anitkabir, AtatĂĽrk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal AtatĂĽrk katika makumbusho ya Anitkabir, AtatĂĽrk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024. Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Ziara yake Rasmi katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024. Kulia ni mweneyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages