LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 10, 2024

UWT YAPONGEZWA KUFANIKISHA IFTAR YA KUMUOMBEA DUA RAIS SAMIA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda akiongoza kupata futari iliyoandaliwa na UWT maalumu kwa ajili ya kumombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Msikiti wa Gadaf jijini Dodoma Aprili 9, 2024. Nyuma yake ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule.
Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab Shaban akiwaongoza waumini wa kiislam kupata futari iliyoandaliwa na UWT.Sheikh Shaban ameipongeza UWT kuwaandalia Iftar hiyo ambayo kwa bahati nzuri ilikuwa ya kuhitimisha mfungo wa Ramadhan.
Mbunge wa Ilemela, Dkt Angeline Mabula (mbele) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angela Kairuki wakishiriki katika tukio hilo.

Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislam wakipata futari.

Baadhi ya viongozi wa Dini ya Kiislam wakifuturu.
Mwenyekiti wa UWT, Chatanda (katikati) akifuturu. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Majule.
Ni wakati wa kupata futari na kufuturu.


Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab Shaban akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Msemaji wake, Sheikh Ahmed Said kuanza dua ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan.
Sheikh Ahmed Said akiongoza dua ya kumuombea Rais Samia. Kushoto ni Wazir wa Madini, ambaye ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.

Chatanda akiwa na Kairuki (kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule wakishiriki dua ya kumuombea Rais Samia.





Chatanda akizungumza baada ya dua ya kumuombea Rais kufanyika ambapo aliwashukuru viongozi wa dini ya kiislam Mkoa wa Dodoma kushiriki na kufanikisha Iftar hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Senyamule  akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson aliyetakiwa kuwa mgeni wa shughuli hiyo lakini hakufika kwa vile alienda kushiriki msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar, Abdulwakili.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) Wilaya ya Dodoma Mjini,  Fatma Hussein akitoa neno la shukrano kwa UWT kuandaa Iftar hiyo.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Dodoma, Zainab Kondo naye akitoa shukrani.

 

Chatanda akiondoka baada ya iftar hiyo ya kumuombea dua Rais Samia kumalizika.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages