LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 23, 2024

KYERWA YAFANYA DUA MAALUMU KULIOMBEA TAIFA

 Na Lydia Lugakila. 

Kyerwa.


Katika kuelekea miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera imefanya dua maalum kuliombea Taifa huku Wananchi Wilayani humo na Watanzania kwa ujumla wakitakiwa kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Dua hiyo maalum imefanyika April 22, 2024 katika Viwanja vya Isingiro Stesheni katika kata ya Isingiro.


Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Zaituni Msofe ambaye amekuwa mgeni rasmi katika dua hiyo amewahimiza WanaKyerwa na Watanzania kwa  kudumisha Muungano huo.


 Bi Msofe ametumia nafasi hiyo kuwataka pia Viongozi wa  Dini  kuliombea Taifa na Viongozi wake kila siku ili amani upendo na mshikamano vitawale zaidi.


Dua hiyo iliongozwa na Viongozi wa Dini ambapo pia iliambatana na zoezi la uzinduzi wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi kumi na nne ambayo itaendelea hadi April 26 mwaka huu.


Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru ni "miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeshikamana na Tumeimarika kwa maendeleo ya Taifa letu"




No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages