LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 18, 2024

DKT NCHIMBI KUTINGA MAKAMBAKO NJOMBE


 


 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapimduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye leo anamalizia ziara yake mkoani Mbeya, baadaye mchana anatinga mkoani Njombe kwa kufanya mkutano wake wa hadhara katika Mji wa Makambako.

Akitokea Mbeya asubuhi hii atasalimia wananchi eneo la Chimala na kufanya mkutano mkubwa wa hadhara eneo la Ubaruku, Lujewa wilayani Mbarali na kuelekea Makambako.

Katika ziara Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.

 Kiongozi huyo mtendaji mkuu wa CCM, atakuwa mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku 10 katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.


Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe na Mbeya, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea leo katika Mkoa  wa Njombe na hatimaye katika Mkoa wa Ruvuma.



No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages