LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 24, 2024

DK SAMIA: TUMIENI HISTORIA ZA TAIFA KUWA KIVUTIO CHA UTALII

Ibrahim Bakari, CCM Blog
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesema wakati umefika sasa watunza kumbukumbu kutumia Historia za taifa kama kivutio cha utalii.

Amesema kama ilivyo mataifa mengine duniani, hutumia histori kama kivutio na ndio maana hugawa vitabu vinavyoeleza historia zao na maeneo ya kuvutia na kusisitiza kuwa kuwa njia ya kuisambaza historia ya Tanzania ni kugawa vitabu kwa wingi.

Akizungumza mjini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Kitabu cha Safari ya Muungano kwa picha leo Aprili 24, 2024,  Dk Samia amesema Uturuki ni kati ya mataifa yanayotumia historia zao kuvutia watalii.

Amesema taifa la Uturuki linapata watalii milioni 28 kwa mwaka wanakwenda kusoma historia tu, na sisi tukijipanga katika eneo hilo, tunaweza kupata watalii kama wenzetu.

Uzinduzi huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Aidha, Rais Samia ametumia nafasi hiyo kuwataka Watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano, tunu walizoachiwa na waasisi wa Muungano na kwamba njia pekee ya kuwaenzi waasisi wa Muungano, ni kufanya kazi kwa bidii.

Akizungumzia kitabu hicho, Rais Dk. Samia alisema kuwa ni njia nzuri itakayodumu na kumbukumbu ya vizazi na vizazi lakini akasema itakuwa vizuri ikitawanywa kwa wingi ili Watanzania na watafahamu mengi ambayo hawayafahamu.

Amesema watatumia nafasi hiyo pia kuvigawa kama zawadi nje ya Tanzania ili nchi ifahamike, inakotoka, ilipo na inakokwenda.

Rais  amesema maadhimisho ya mwaka huu yanakwenda sanjari na falsafa yake ya 4R na kwamba kila kilichofanyika kinashabihiana na falsafa hiyo.

Awali Rais Samia ambaye alitaka vitabu alivyozindua vitafsiriwe kwa Kiswahili, ametunuku Nishani za Muungano kwa watumishi mbalimbali kutokana na utumishi uliotukuka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein vitabu vya Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages