Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi, ameitaka Jumuiya ya Vijana wa Chama hicho (UVCCM) na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga Mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa Sababu ameonesha Uzalendo kwa kufanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo Wananchi bila kuangalia Itikadi zao.
Balozi Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam wakati wa Futari iliyoambatana na Dua Maalum ya kumuombea Dkt Samia ili aendelee kutimiza Majukumu yake vizuri kwa Watanzania, ambayo iliandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammed Kawaida na Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Jokate Mwegelo.
"Niwapongeza kwa moyo wenu wa kuwatafuta Watoto yatima na kukaa nao ili kufutari nao pamoja, katika Siku hii ya Dua maalum kwa ajili ya kumuombea Rais wetu na nchi yetu kwa Ujumla, hili ni Jambo kubwa sana na tunamuomba mungu apokee dua zetu" amesema Dkt Nchimbi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇