LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 25, 2024

DC KOBYA, DED MICHUZI WAWATAKA WANANCHI IFAKARA KUCHUKUA TAHADHARI, KUONDOKA MAENEO YALIYOFURIKA MAJI

Mkuu wa Wilaya  ya Kilombero Dustan Kyobya na Mkurugenzi wa Ifakara Mji  Zahara Michuzi  wamewataka wananchi  kuchukua tahadhari mapema na kuondoka maeneo yote yaliyojaa maji.


Viongozi hao wametoa agizo hilo leo Aprili 25, 2025, baada ya kufika na kukagua athari eneo la kingo za mto Lumemo ambao umejaa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuleta mafuriko kwenye makazi na taasisi za umma na binafsi.


Kutokana na mvua hizo baadhi ya shule zimelazimika kufungwa kwa muda mpaka maji yatakapopungua.


Timu za uokoaji  zimepata boti kutoka  TAWA na zinaendelea na doria ya nyumba kwa nyumba kuokoa wananchi.


Nyumba nyingi bado zimezungukwa na maji, hivyo timu za uokoaji zikiongozwa na Kamanda wa zima moto wa wilaya kamanda Haji, Skauti, Msalaba Mwekundu na Halmashauri zinaendelea na doria za nyumba kwa nyumba kuokoa wananchi walioshindwa kutoka majumbani.








No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages