LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 3, 2024

CCM YAWATEUA MONGELLA KUWA NAIBU KATIBU MKUU-BARA, MAKALLA MWENEZI, ALI HAPI WAZAZI, MWENGELO UVCCM

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kikao chake Maalum cha Halimashauri Kuu ya Taifa (NEC), kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kimemteua Amoss Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, kuchukua nafasi iliyoachwa na Paul Makonda aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.

Kikao hicho pia kimemteua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, kuziba nafasi iliyoachwa na Anamringi Macha ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, huku kikimteua Ally Salum Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi  kuchukua nafasi iliyoachwa na Gilbert Kalima aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mkinga.

Pia katika kikao hicho aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Jokate Mwengelo ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Fakii Raphael Lulandala aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo imesema, kikao hicho NEC imezipongeza Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. Samia na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages