Na Hemed Munga, Singida
VIONGOZI wa
wanawake wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) mkoani Singida wamemuahidi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kumchagua
kwa kishindo ifikapo 2025 kwa sababu aliyowafanyia ni makubwa.
Akizungumza
katika kongamano la kumshukuru na kumpongeza Rais huyo kwa uongozi bora
na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake,
lililofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba
mjini Kiomboi mkoani hapa, Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, (UWT) ambae
anawawakilisha wanawake wa mkoa huo, Grace Mkoma alisema Rais Dk. Samia
Suluhu Hassan amesababisha wanawake hivi sasa wanajidai huku wakinababa
wakikaa nyuma yao.
"Ndugu
zangu Rais wetu ametuheshimisha sana, ametufanya wanawake tutembee
kifua mbele, ninampongeza sana Mama yetu, tunakuahidi kukupa maua yako
ifikapo 2025," ameahidi Grace.
Aidha,
amebainisha kuwa wakati wa nyuma walikua wakisoma kwa kutumia mwanga wa
kibatali lakini leo hii umeme umefika kila pahali ikiwemo barabara ya
lami kufika mpaka mlangoni kwao.
Mbali
na hayo, Grace aliongeza kuwa wanawake wa wilaya na mkoa huo, walikua
na shida ya maji lakini leo hii kunamabomba majumbani kwao.
"Hakika
hii ni kazi ambayo imefanywa na Mwanamke wa shoka Rais Dk. Samia Suluhu
Hassan, hivyo tunakila sababu ya kujivunia mwanamke huyu kwa
kutuheshimisha na kusimama kweli kweli:
"Ninakila
sababu ya kusema Rais Dk. Samia anatosha na 2025 wanawake wa mkoa wa
Singida tunakwenda na Samia kumpa mitano tena," amesisitiza.
Katika
hatua nyingine, Grace amemshukuru na kuompongeza Mbunge wa jimbo hilo,
ambae ni Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba kwa kulisemea jimbo hilo,
hatimaye likapata fedha zilizoleta maendeleo makubwa.
"Mbunge
wetu ni baba wa watoto wengi, kaka wa wadogo wengi na mlezi wa wengi,
hakika yeye ni baba mwema sana, hivyo naye tutampa mitano tena,"
amesema.
Kwa upande wa
Mwenyekiti wa UWT mkoani hapa, Martha Kayaga aliushukuru uongozi wa
Mtakwimu Mkuu wa Serikali unaoongozwa na Dk. Albina Chuwa kwa kuendelea
kutekeleza agizo la Rais Dk. Samia kutoa mafunzo ya usambazaji na
uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 kwa mkoa wa
Singida.
Amesema mafunzo
hayo yanawaelimisha namna bora ya kutumia matokeo hayo kwa lengo la
kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.
Mbali
na hayo, kwa sababu wao ni viongozi yatawasaidia kuandaa bajeti na
ratiba za kazi zao za kila siku ikiwemo uandikishaji unaoendelea.
Aidha,
aliahidi kuwa watayatumia mafunzo hayo hususan katika kipindi hichi
ambacho wanaendesha uandikishaji kidigitali kujua takwimu kutokana na
visimbuzi wanavyotumia.
Mjumbe
wa Baraza Kuu Taifa, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambae
anawawakilisha wanawake wa mkoa wa Singida, Grace Mkoma akimshukuru na
kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya uongozi bora
ndani ya miaka mitatu, leo katika kongamano lililofanyika katika Ukumbi
Mkubwa wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba, mjini Kiomboi. (Picha na
Hemedi Munga)
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Warda Obathany akiwasihi
wanawake kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutoa maoni kuhusu Dira
ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2050, leo katika kongamano la
kumpongeza na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya
uongozi bora ndani ya miaka mitatu, lililofanyika katika Ukumbi Mkubwa
wa Halmashauri hiyo, mjini Kiomboi. (Picha na Hemedi Munga)



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇