LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 25, 2024

KOMREDI MWAJABU MBWAMBO AWAJENGEA UWEZO MABINTI KATIKA MASUALA YA UONGOZI ILI KUJIANDAA KUWA VIONGOZI BORA WENYE MAADILI MEMA KATIKA NYANJA TOFAUTI KATIKA TAIFA LA TANZANIA

Ahimiza Mabint Dar es salaam kujianda kwa kujijenga kuwa viongozi wa baadae kuhakikisha wana ujuzi wa kutosha katika eneo wanalolifanyia kazi, wahakikishe wanapata elimu stahiki, kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, kutafuta fursa, kutengeneza mtandao wa mabint katika nyanja tofauti, na kuwa mstari wa mbele kujitolea, na kuhakikisha mabint wananyanyuana wenyewe kwa wenyewe._ 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es salaam Ndugu. Mwajabu Rajabu Mbwambo, ameshiriki katika kongamano la  "_Thamani ya Bint  Mwenye Ndoto 2024_" lililoandaliwa na asasi isiyo ya serikali Voice of Eagle Tanzania chini ya CEO wa Bwana Meshack  Mafyeko. Katika Kongamano  Komredi Mwajabu ametoa Mada Fursa ya Bint mwenye ndoto na Uongozi. Mada hiyo imegusa nukta zifuatazo:
Sifa za kiongozi
1. Awe na ufahamu katika maeneo yafuatayo;
       - Taasisi/ kikundi  
         biashara anayoongoza
       - Malengo 
       - Mipango
       - Maono
       -Mazingira
       - Fursa
       - Changamoto
      
2. Awe na hofu ya mungu na kutenda majukumu yake kwa uadilifu.
3. Awe na maadili mema. Asigombanishe, kufitinisha, umbeya, majungu, chuki, wivu na mwizi.
4. Awe mwaminifu 
5. Uwezo wa kujifunza kila mara, kuongeza ufanisi wake na kujifunzs kwa waliofanikiwa
6. Awe Mstahamilivu/ Resilience
7. Kupokea ushauri na kushauri
*Cde Mwajabu* amewajuza kwamba ili kufikia  Malengo ni lazima kujiendeleza wao binafsi kwa kupata mbinu za kuongoza kwa kuangalia yafuatayo;
1. Kutambua vipawa walivyo navyo na madhaifu yao ili kujiboresha na kuwa weled zaidi
2. kufahamu aina ya uongozi kulinga na eneo walilojikitana nalo
3. kutengeneza na kutanua wigo wa networking.
4. kuwa Role Model wa kujifunza na kupata ushauri wake
5. wahakikishe kila siku wanajifunza mbinu na mikakati ya uongozi.

Cde Mwajabu amewapa mfano mzuri kwa Tanzania Role Model aliyepo Madarakani Rais *Dr Samia Suluhu Hassan* na falsafa ya 50/ 50 na amehakikisha ameweka mawaziri na manaibu wanawake, makatibu na manaibu katibu wa kuu wanawake, wakuu wa mikoa na wilaya na makatibu tawala mikoa na wilaya, wakurugenzi na viongozi mbalimbali wanawake katika taasisi za serikali.

Cde. Mwajabu amepongeza Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa mambo mengi aliyofanya ndani ya kipindi cha miaka mitatu kwa kuwa kiongozi bora wa kuacha alama na kusimamia falsafa yake ya 4Rs
na kunyanyua wanawake wenye uwezo kwa kuwateua katika nafasi za juu za uongozi ili kuleta mabadiliko.

"Binti unatakiwa ujipambanue kwa kujitambua  kuwa Personal Branding yako ni
1. Tabasamu lako ndio Logo  yako
2. Muonekano wako ndio Business Card yako
3. Jinsi unavyofanya wengine wajisikie katika uongozi wako ndio Trade mark yako".

Ndugu. Mwajabu Mbwambo
Mweyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es salaam.

Ubungo  Mlimani City
 23 Machi, 2024

#Thamani yabinti mwenye Ndoto 2024
#Dar es salaam
# UwtImara Jeshi la Mama Kazi iendelee



No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages