LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 27, 2024

SHIRIKISHO LA UMOJA WA MACHINGA MKOA WA PWANI : RAIS SAMIA UMETUHESHIMISHA



Na Dismas LYASSA

HUKU Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan akiwa ametimiza miaka mitatu tangu kuingia madarakani wafanyabiashara wadogo mkoa wa Pwani wanasema miaka mitatu imekuwa ni faraja kwao.

"Sote ni mashahidi wala huhitaji kwenda chuo kikuu kufanya utafiti...kwamba Rais Dk Samia ametuheshimisha sana machinga... sote ni mashahidi kwamba tulikuwa tukiona mgambo wakisumbua machinga, sasa mambo kama haya hayapo, machinga tunafanya kazi kwa amani," anasema Phillemon Maliga, MWenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) Mkoa wa Pwani.

Akihojiwa na Msemaji na Afisa Habari wa SHIUMA Mkoa wa Pwani, Dismas LYASSA, Mwenyekiti huyo wa SHIUMA Mkoa wa Pwani alisema Watanzania wana macho wanaona kwa dhati namna Serikali ya awamu ya sita inavyowaheshimisha machinga kwa namna mbalimbali.

“We uliona machinga wanakuwa na ofisi… Lakini mama Samia katupatia fedha tumejenga ofisi ya Machinga Mkoa wa Pwani ili machinga tuwe tunakutana na kujadili mambo yetu,” anasema Maliga na kuongeza kuwa heshima hii kubwa imepatikana kupitia Dk Samia na machinga kwa ujumla wanaridhishwa na uongozi wa Serikali ya awamu ya sita.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages