Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi huku akimteua aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Itikadi na Uenezi Paul Makonda kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Taarifa ya Ikulu, imesema, Makonda anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo wa Arusha John Vianney Mongella ambaye kwa mujibu wa Ikulu atapangiwa kazi nyingine.
Pia, Rais amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius John Ndejembi, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kuchukua nafasi ya Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wengine ni Kanali Evans Alfred Mtambi ambaye Rais amemteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akitoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Said Mohamed Mtanda akihamishwa kutoka Mkoa wa Mara kwenda Mkoa wa Mwanza kuchukua nafasi ya Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Taarifa imesema, Rais amemteua pia Zainab Athuman Katimba, kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuchukua nafasi ya Deogratius John Ndejembi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.
Pia Rais amemteua Daniel Baran Sillo, kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuchukua nafasi ya Jumanne Abdallah Sagini, ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.
Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi naye Rais amemhamisha kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari huku Kundo Andrea Mathew akimhamisha kutoka Wizara hiyo kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.
Taarifa ya Ikulu imeendelea kueleza kuwa Rais amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Fakii Raphael Lulandala, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, huku akimteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya wa Wazazi ya CCM Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
Pia taarifa imesema, Rais amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Mary Ngelela Maganga akimhamisha kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Katika Uteuizi huo, pia Rais amemteua aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dk. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kucukua nafasi ya Agnes Kisaka Meena ambaye amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.
Pia Rais memteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dk. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchu nafasi ya Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.
Wakati huohuo, Rais amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi, na pia kumteua Balozi Dk. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango.
"Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuu utafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam", taatifa ya Ikulu, imesema.
Dk. Asha-Rose Migiro
Deogratius John Ndejembi |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇