Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mama Siti Mwinyi, Mjane wa Rais Mstaafu awamu ya pili Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kupokea mwili wa hayati Mzee Mwinyi, jana, tarehe 01 Machi 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi wakiomba Dua mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu awamu ya pili Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi, lilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar jana, Machi Mosi, 2024.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇