--------------------------------------------------
Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Wakati Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akitimiza miaka mitatu tangu alipoapishwa Machi 19, 2021 kuwa Rais wa Awamu ya Sita, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imekiri kwamba juhudi na ubunivu wa Rais huyo vimezaa mafanikio lukuki kwenye sekta ya uhifadhi na utalii nchini.
Imesema, miongoni mwa juhudi aliofanya Rais Dk. Samia katika miaka yake mitatu tangu awe Rais ni kutoa fedha za kuendeleza miundombinu ya uhifadho na utalii na kubuni fursa za kuitangaza sekta hiyo katika masoko ya Kitaifa na Kimataifa hasa kupitia Filamu ya the Royal Tour.
Hayo yamesemwa na Kamisha wa Uhifadhi wa TAWA, Kamishna Mabula Misungwi Nyanda, wakati akitoa wasilisho la mafanikio ya TAWA kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita Dk. Samia, katika Kikao Kazi na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam, leo, Machi 18, 2024.
Amesema, miongoni mwa mafanikio ambayo TAWA imeyapata katika kipindi hicho ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, akisema; Idadi ya watalii wa picha na uwindaji imeongezeka kutoka kutoka 37,684 mwaka 2020/21 hadi 166,964 mwaka 2022/23 na watalii 116,529 hadi Februari 2024, Wawindaji kutoka 355 mwaka 2020/21 hadi wawindaji 787 mwaka 2022/23 na wawindaji 481 hadi Februari mwaka 2024.
Kamishna Nyanda amesema pia meli za Kimataifa za utalii kutembelea eneo la Kihistoria Kilwa zimeongezeka kutoka meli 4 zilizokuwa na watalii 400 mwaka 2020/21 hadi meli 8 zenye watalii 925 na pia TAWA imeuza vitalu kwa Mnada wa Kieletroniki na kuanza utekelezaji wa Uwekezaji Mahiri.
Alisema miongoni mwa mafanikio yaliyoletwa na Filamu ya Royal Tour ni mwitikio mkubwa wa wawekezaji katika mnada wa vitalu vya utalii ambapo jumla ya vitalu 66 vimeuzwa na mapato ya jumla ya Dola za Kimarekani 8,277,000 zilikusanywa ikilinganishwa na Dola 2,405,000, endapo vitalu hivyo vingeuzwa kwa njia ya utawala ikiwa ni ongezeko la Dola 5,872,000.
Pia Kamishna huyo amesema, Serikali ilikamilisha taratibu za uwekezaji kwa ajili ya kusaini mikataba ya uwekezaji mahiri katika Vitalu vya Ikorongo, Grumeti, Maswa Mbono, Maswa Kimani, Maswa North, Mkungunero na Selous LL1. Mikataba saba ilisainiwa Januari 2024 ambapo kupitia mikataba hiyo Serikali itapata Dola za Marekani milioni 312. 25 kwa kipindi cha miaka 20 sawa na wastai wa Dola za Marekani milioni 15.5.
Amesema, kufuatia juhudi hizo idadi ya vitalu uwindaji vyenye wawekezaji imeongezeka kutoka kutoka 59 hadi 68 na pia kusainiwa na kuanza utelelezaji wa Mikataba ya uwekezaji mahiri –SWICA jumla ya Dola za Marekani 2,773, 000 sawa na Sh. Bilioni 7.01 zimekusanywa tangu kusainiwa kwa mikataba hiyo ya SWICA Januari 3 mwaka 2024.
Kamishna amesema, mafanikio zaidi ni kwamba ukusanyaji wa maduhuli kupitia vyanzo mbalimbali umepaa na kuifanya TAWA kuchangia katika Mfuko Mkuu wa Serikali, ambapo Jumla ya kiasi cha sh. Bilioni 184.74 zimekusanywa kati ya mwaka 2020/21 hadi 2024 March 8.
Taarifa Kamili iliyowasilishwa na Kamishna Nyanda,👇
Picha za kikao kazi hicho.👇
Kamisha wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Kamishna Mabula Misungwi Nyanda, akitoa wasilisho la mafanikio ya TAWA kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita Dk. Samia, katika Kikao Kazi na Wahariri wa habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam, leo, Machi 18, 2024.
Mhariri Abdallah Majura akuliza maswali
Mhariri Manyerere Jacton akiuliza maswali.
Baadhi ya Viongozi wa TAWA wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa Habari wakiwa kwenye kikao hicho.
Baadhi ya Wahariri, Waandishi wa Habari na Maofisa wa TAWA wakiwa kwenye kikao hicho.
Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa Habari wakiwa kwenye kikao hicho.Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Nevil Meena akizungumza kwenye kikao kazi hicho.Mkuu wa Habari na Mahusano wa TAWA akizungumza katika kikao Kazi hicho.























No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇