Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akizungumza wakati wa kutoa salaam za CCM za mshikamano kwenye Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (FLMS), leo Jumatatu, Machi 18, 2024. Mkutano huo unaofanyika katika Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe, umewakutanisha Makatibu Wakuu wengine wa vyama hivyo rafiki, ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia) Komredi Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Komredi Fikile Mbalula, Komredi Roque Silva Samuel (FRELIMO - Msumbiji), Komredi Paulo Pombolo (MPLA - Angola), Komredi Kavis Kario (BDP – Botswana) na Komredi Albert Mpofu (ZANU – PF - Zimbabwe), ambaye ni mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano huo.
Mkutano wa 11 wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (FLMS), unaowakutanisha wajumbe wake, ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia), Komredi Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Komredi Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Komredi Roque Silva Samuel, Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA (Angola), Komredi Paulo Pombolo, Katibu Mkuu wa Chama cha BDP (Botswana), Komredi Kavis Kario na Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU – PF (Zimbabwe), Komredi Albert Mpofu, (mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano), ukiendelea kujadili agenda, leo Jumatatu, Machi 18, 2024, katika ukumbi ulioko Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe, unakofanyikia.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akijadiliana jambo na wajumbe wa msafara wake aliombatana nao kushiriki Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (FLMS), leo Jumatatu, Machi 18, 2024. Kutoka kushoto ni Gilbert Kalima (Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi), Fack Lulandala (Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM – UVCCM), akifuatiwa na Tunu Juma Kondo (Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake – UWT – Zanzibar). Mkutano huo unaofanyika katika Mji wa Victoria Fall, nchini Zimbabwe, umewakutanisha Makatibu Wakuu wengine wa vyama hivyo rafiki, ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia) Komredi Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Komredi Fikile Mbalula, Komredi Roque Silva Samuel (FRELIMO - Msumbiji), Komredi Paulo Pombolo (MPLA - Angola), Komredi Kavis Kario (BDP – Botswana) na Komredi Albert Mpofu (ZANU – PF - Zimbabwe), ambaye ni mwenyeji na mwenyekiti wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja, leo Jumatatu, Machi 18, 2024, pembezoni mwa siku ya kwanza ya Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, unaofanyika katika Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe. Makatibu Wakuu wengine pichani, (kutoka kulia) ni Komredi Roque Silva Samuel (FRELIMO - Msumbiji), Komredi Paulo Pombolo (MPLA - Angola), Komredi Albert Mpofu (ZANU – PF - Zimbabwe, mwenye suti), Komredi Sophia Shaningwa (SWAPO – Namibia) na Komredi Fikile Mbalula (ANC – ANC).
Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi (kushoto) kwenye picha
ya pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia) Komredi Sophia
Shaningwa (katikati) na Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini),
Komredi Fikile Mbalula (kulia), wakionesha alama ya salaam za CCM, Chama
cha ANC na Chama cha SWAPO, leo Jumatatu, Machi 18, 2024, pembezoni mwa
siku ya kwanza ya Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya
Ukombozi Kusini mwa Afrika, unaofanyika katika Mji wa Victoria Falls,
nchini Zimbabwe. Makatibu Wakuu wa Vyama wengine wanaoshiriki mkutano
huo ni pamoja na Komredi Roque Silva Samuel (FRELIMO - Msumbiji),
Komredi Paulo Pombolo (MPLA - Angola), Komredi Kavis Kario (BDP –
Botswana) na Komredi Albert Mpofu (ZANU – PF - Zimbabwe), ambaye ni
mwenyeji wa mkutano huo. (MAELEZO NA PICHA ZOTE NA AHMAD MICHUZI- OFISI YA KATIBU MKUU WA CCM).
Your Ad Spot
Mar 18, 2024
Home
featured
siasa
BALOZI DK. NCHIMBI KATIKA MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, LEO
BALOZI DK. NCHIMBI KATIKA MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot






No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇