Na Is-haka Omar, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimeonya kuwa kitawachukulia hatua kali za kisheria wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaotumia vibaya majukwaa ya kisiasa kumdhalilisha na kumdhihaki hadharani Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Mohamed Said Dimwa, wakati akizungumza na wanachama na viongozi wa Chama Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanatumia vibaya uhuru wa kutoa maoni na badala yake wanatoa kauli za kumdhalilisha Rais wa Zanzibar Dk. Mwinyi huku wakipandikiza kauli za uchochezi kwa wananchi.
Dk. Dimwa, aliviomba Vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa hao na watu wengine wanaovunja sheria kwa makusudi kwa kumdhalilisha Rais wa Zanzibar.
Pia amevitaka vyombo hivyo vya ulinzi kwenda mbali zaidi kwa kuthibiti upotoshaji unaondikwa katika mitandao ya kijamii nchini kwa lengo la kumdhalilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
“Juzi Chama Cha ACT-Wazalendo wamefanya mapokezi ya Viongozi wao lakini jambo la kusikitisha mikutano yao kwa Unguja na Pemba imepambwa na kauli chafu zilizojaa chuki, visasi, uongo na fitna dhidi ya Rais wetu Dk. Hussein Mwinyi, hatuwezi kuvumilia utovu huo wa nidhamu kwani haukubaliki kisiasa, kidini na kitamaduni.
Tabia hizo zinafanya tuanze kutilia mashaka kama kweli wenzetu wana nia ya dhati ya kuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) au wana ajenda zao binafsi kuirejesha Zanzibar katika machafuko ya kisiasa”, alihoji Dkt.Dimwa.
Katika maelezo yake Dk. Dimwa, amesema CCM itaendelea kulinda kwa vitendo heshima,hadhi thamani ya Rais wa Zanzibar na wasaidizi wake kwani wapo katika mamlaka yanayotokana na Chama Tawala cha CCM kupitia ridhaa halali ya uchaguzi wa Kidemokrasia chini ya matakwa ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Naibu Katibu Mkuu huyo Dk. Dimwa, alisema wananchi wanahitaji siasa za kuvumiliana na ustaarabu sambamba na kuona wananufaika kiuchumi na kijamii huku nchi ikipiga hatua kubwa za maendeleo.
Sanjari na hayo,aliweka wazi kuwa vyama vya siasa Zanzibar vimepoteza muelekeo na mvuto kwa wananchi kutokana na kasi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Kupitia mkutano huo Dkt.Dimwa,aliwasihi Wanachama na Viongozi wa CCM kujibu hoja kwa hoja huku wakitangaza na kuhamasisha kwa kasi kubwa mambo yaliyotekelezwa na Serikali Mijini na Vijijini kwa maslahi ya wananchi.
Your Ad Spot
Mar 12, 2024
Home
featured
siasa
DK. DIMWA: KOMENI KUMDHALILISHA, KUMDHIHAKI RAIS DK. MWIMYI, CCM ITAWACHUKULIA KISHERIA
DK. DIMWA: KOMENI KUMDHALILISHA, KUMDHIHAKI RAIS DK. MWIMYI, CCM ITAWACHUKULIA KISHERIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇