Official CCM Blog, Dar es Salaam
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi kilichotokea jana, Februaei 29, 2024, katika Hospitali ya Mzena, alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Kimesema, Mzee Mwinyi atakumbukwa kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii aliyoyaongoza akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia (1985-1995) na pia jitihada zake kubwa katika mabadiliko ya kiutendaji, kiuendeshaji na kimfumo ndani ya Chama alipokuwa Mwenyekiti (1990-1996)
"Sanjari na hayo Mzee Mwinyi atakumbukwa daima kwa mchango wake katika kusaidia kujenga umoja wa kitaifa na kulinda Muungano ambao ni mojawapo ya tunu zetu za taifa, wakati wa utumishi wake serikalini.
Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kumuenzi Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa yale yote mema aliyotuusia na kututendea. Tunamuombea apumzike kwa amani na tunawambea familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu", amesema Katibu Mkuu wa CCM katika taarifa aliyosaini na kutumwa kwenye vyombo vya habari.
Your Ad Spot
Mar 1, 2024
CCM: MZEE MWINYI ATAKUMBUKWA KWA MAGEUZI SERIKALINI, MABADILIKO NDANI YA CCM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇