Zimbabwe, leo
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amewasili nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa 11 wa siku tatu wa Makatibu Wakuu wa Vyama Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (FLMS), utakaoanza kesho Machi 17, 2024 katika mji wa Victoria Falls nchini humo.
Katika msafara wake, Katibu Mkuu Balozi Dk. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Gilbert Kalima, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM), Fack Raphael Lulandala, na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Zanzibar, Tunu Juma Kondo.
Mkutano huo unalenga kujadili agenda mbalimbali zinazohusu urafiki na uhusiano wa vyama hivyo ambavyo vyote viko madarakani, vikiongoza Serikali na Nchi husika.
Mbali ya Chama Cha Mapinduzi, vyama vingine vinavyoshiriki mkutano huo ni pamoja na mwenyeji ZANU – PF (Zimbabwe), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia), FRELIMO (Msumbiji), ANC (Afrika Kusini) na Botswana Democratic Party (BDP – cha Botswana).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akisalimiana na kuzungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia), Komredi Mama Sophia Shaningwa walipokutana mara baada ya kuwasili nchini Zimbabwe, leo mchana Machi 17, 2024, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, utakaofanyika nchini humo.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇