Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea Ofisi za Vyombo vya Habari minavyomilikiwa na Chama, na Kikundi cha hamasa cha Tanzania One Thetre (TOT) cha CCM, kuona hali ya utendaji, vitendea kazi na baadaye kuzungumza na viongozi na wafanyakasi wa taasisi hizo, Alhamisi, Machi 7, 2024.
Balozi Dk. Nchimbi ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Paul Makaonda, ambaye ndiye msimamizi wa Taasisi hizo, amefanya ziara hiyo ikiwa ni ya kwanza tangu ateuliwe na Kikao Maalum cha NEC, kilichofanyika Januari 15, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.
Kufuatia ziara hiyo, pia Makonda imekuwa ni kwa mara ya kwanza kufika kwenye taasisi hizo tangu ateuliwe na NEC kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM katika kikao kilichofanyika Oktoba 22, 2023, Jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo Balozi Dk. Nchimbi alianza kutembelea Ofisi ya TOT, Ofisi ya CCM Mwananyamala Mwinjuma, na kuzungumza na wafanyakazi wakiongozwa na Mkurugenzi Khadija Omar Kopa na baadaye akaenda Ofisi za Africa Media Group Limited inayoendesha kituo cha televisheni cha Channel ten na Magic fm.
Baada ya kutoka Africa Media Group Ltd alienda Ofisi za Uhuru Publications Ltd, inayochapisha Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Uhuru la Kijani, kisha akaenda Peoples' Media Ltd inayoendesha kituo cha Radio cha Uhuru fm.
Balozi Dk. Nchimbi alihitimisha ziara hiyo kwa kuzungumza na viongozi na wafanyakazi wa Uhuru Publications Ltd, Uhuru FM na Uhuru Media (UMG), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Katika kikaokazi hicho, Balozi Dk. Nchimbi aliwapa fursa wafanyakazi kueleza bila hofu changamaoto zinazowakabili wao na taasisi zao, ili hatimaye zitafutiwe ufumbuzi, akisisitiza kuwa ufumbuzi wenyewe hautahusiana na miujiza bali uhalisia.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wafanyakazi wa Vyombo vya Habari minavyomilikiwa na Chama, katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbu wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, Jumatano, Machi 7, 2024. Pamoja naye ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Paul Makonda.
Balozi Dk. Nchimbi akizungumza na Viongozi wa Uhuru Publications Ltd (UPL) katika Ofisi za UPL, Lumumba Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Ramadhan Mkoma. na aliyeketi ni Mwenezi wa CCM Paul Makonda.
Mwenezi Makonda akiwa amesimama kumsikiliza Balozi Dk. Nchimbi wakati akielekeza jambo. wakati akizungumza na Viongozi wa Uhuru Publications Ltd (UPL) katika Ofisi za UPL, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Balozi Dk. Nchimbi akipiga 'shoto kulia' na Mwenezi Makonda kwenda Ofisi za Uhuru fm baada ya kutoka UPL.Balozi Dk. Nchimbi akisalimia baadhi ya wananchi waliojitokeza kado kumuona wakati akitoka UPL kwenda Uhuru fm wakati wa ziara hiyo.Balozi Dk. Nchimbi akisalimiana na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Uhuru fm, Amina Aziz alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, zilipo ofisi za Uhuru fm.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Uhuru fm, Amina Aziz katika studio za Uhuru fm.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akimsikiliza kwa makini Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Uhuru fm, Amina Aziz.
Mwenezi Paul Makonda akizungumza na kumkaribisha Balozi Dk. Nchimbi kuzungumza na wafanyakazi.
![]() |
| Balozi Dk. Nchimbi akizungumza na Wafanyakazi. |
![]() |
| Wafanyakazi wakiwa kwenye kikao hicho. |
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na baadhi ya watangazaji wa Magic Fm, waliokuwa chumba cha kutangazia, alipofanya ziara katika Ofisi za Africa Media Group Limited,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Watumishi wa Tanzania One Theatre (TOT).Mkurugenzi wa TOT Khadija Kopa akizungumza.










No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇