LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 13, 2024

WAZIRI WA ZAMANI BALOZI DK. KAMALA AFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM

Official CCM Blog, Dar es Salaam
Balozi Mstaafu na Waziri wa zamani Wizara ya Afrika Mashariki Dk. Deodorus Buberwa Kamala amefariki dunia, katika hospitali ya Mzeena, Kijitonyama, Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dk. Kamala amefariki katika umri wa miaka 55, akiwa amewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Nkenge wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kuanzia mwaka 2000 hadi 2010, na mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki na baadaye Waziri Kamili wa wizara hiyo mwaka 2008 hadi 2010

Mwaka 2011 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Uholanzi ambako alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2015 aliporejea kuwa Mbunge hadi mwaka 2020.

Waziri wa zamani Balozi Dk. Diodorus Kamala enzi za uhai wake.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages