LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 12, 2024

BODI YA ZHC ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI YA NHC DODOMA

Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Nyumba Zanzibar wakitembelea mradi wa nyumba 100 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambazo tayari zimeuzwa eneo la Chamwino, Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),  Hamad Abdallah akielezea mbele ya wajumbe wa Bodi ya Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC),kuhusu maendeleo ya mradi wao wa kisasa wa majengo ya Morocco Square uliopo jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo umefanya ziara ya kubadilishana uzoefu na NHC ikiwemo kutembelea baadhi ya miradi ya NHC iliyopo Dodoma.


Ujumbe huo kutoka Zanzibar umetembelea mradi wa nyumba 100 za NHC zilizopo eneo la Chamwino ambazo zote tayari zimeuzwa. Pia wametembelea miradi ya ujenzi wa majengo ya wizara 10 unaofanywa na NHC pamoja mradi wa nyumba zaidi ya 300 katika eneo la Iyumbu.


Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Doroth Mwanyika  akizungumza alipokuwa akiukaribisha ujumbe wa Bodi ya ZHC wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu katika Ofisi za NHC jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya ZHC.
Mwanyika akiongoza kikao hicho



Meneja Habari na Mawasiliano wa NHC, Muungano Saguya akiratibu kikao hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Abdallah akielezea kuhusu utendaji wa shirika hilo\.
Ujumbe wa Bodi ya NHC ukitembelea mradi wa nyumba 100 za NHC zilizopo Chamwini Dodoma.





 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages