LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 4, 2024

SERIKALI WILAYANI KYERWA YAMPONGEZA RAIS SAMIA KUPAA KWA ZAO LA KAHAWA

 

Na Lydia Lugakila, Kyerwa.


Serikali Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera imetoa pongeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia  Suluhu Hassan kwa namna alivyokubali kuhakikisha vyama vya Msingi vinajitegemea lakini pia kutegemea Biashara ya mnada ambayo imeweka bei ya Kahawa juu na kuwaongezea Wananchi kipato chao.


Pongezi hizo zimetolewa kupitia taarifa ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bahati Henerco katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili 2023/2024 kilichofanyika Wilayani humo.


Henerco amesema kuwa jitihada za Rais Samia ni kubwa sana katika zao hilo la Kahawa kwa Wilaya hiyo huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuendelea kuhamasisha Wananchi kulima kahawa kwa wingi kwani tayari Rais Samia kaweka utaratibu mzuri na rafiki kwa Wakulima hao.


Amesema kuwa malengo yote ya uzalishaji wa kawaha kwa Halmashauri hiyo ni kutaka kutoka tani wanazozalisha hadi tani elfu 60 ndani ya miaka mitano ijayo ili kufika mwaka 2030 waweze kwenda zaidi mpaka tani laki 1 ambazo wakizalisha  kama bei inaweza ikawa hiyo waionayo Wananchi wa Wilaya hiyo Wana uwezo wa kuingiza mpaka shilingi Bilioni 300.


Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ameongeza kuwa kwa sasa wanazalisha tani elfu 30 mpaka 45 ambazo kwa mwaka 2000 na kurudi nyuma  tani elfu 30 zilikuwa zinaingiza shilingi Bilioni 30 huku tani elfu 45 ziliingiza shilingi Bilioni 45.


"Kwa miaka hii miwili baada ya kuwa imetangazwa biashara za mnada kwa mwaka huu tumekusanya tani elfu 30 ambazo zimewaingizia Wananchi zaidi ya shilingi Bilioni 90 kutoka Bilioni 30 ambapo kwa uchumi wa kawaida uchumi wa Wilaya hii umekua kwa kasi kubwa" alisema Henerco.


Aidha ameongeza kuwa kwa mwaka 2023 walizalisha tani elfu 38 ambazo kwa bei ya Kahawa waliingiza zaidi ya Bilioni 80 tofauti na Bilioni 38 zilizokuwa zinaingizwa hivyo ni ongezeko kubwa kwa zao hilo.


Hata hivyo aliwapongeza wote walioshiriki katika maendeleo hayo makubwa huku akiomba biashara ambayo watu walizoea kuendesha ya magendo kwa maana ya Kahawa kwenda nje ya Nchi Sasa irudishwe ndani ili kuhakikisha kila mkulima kahawa yake inauzwa kwenye vyama vya Msingi na inaboreshwa na bei kuwa nzuri ili Serikali ikae sawa na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo yawe sawa sawa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages