TAARIFA YA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE. BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA KWA WAANDISHI WA HABARI JUU YA MAANDALIZI YA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHERIA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA UTAKAOFANYIKA ZANZIBAR TAREHE 4-8
MACHI, 2024
Ndugu Waandishi wa Habari,
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa
kutujalia neema ya uhai na kutuwezesha kukutana nanyi waandishi wa
habari katika kikao hiki kinachuhusu taarifa ya maandalizi ya mkutano wa
mawaziri wa sheria wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola
kitakachofanyika Unguja- Zanzibar kuanzia tarehe 4 mpaka 8 Machi, 2024
Nichukue nafasi hii kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuridhia
mkutano huu kufanyika nchini kwetu. Hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu
kuwa mwenyeji wa Mkutano huu mkubwa unaotarajiwa kuwaleta nchini kwa
pamoja mawaziri wa Sheria wa nchi 56 wakiambatana na maofisa wao
waandamizi. Niwashukuru viongozi wote ambao wameshirikiana bega kwa
bega katika kuhakikisha wanasimamia maandalizi ya kazi hii kutoka katika
pande zote mbili za Muungano yaani Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.
Lakini pia niwapongeze wataalam wote ambao hata tunavyoongea wapo
wakiendelea na maandalizi ya mkutano huu mkubwa ambao pamoja na
mambo mengine utatoa fursa ya kuitambulisha nchi yetu na vivutio vyake.
Ila kwa namna ya pekee niendelee kuwapongeza na kutoa shukrani zangu
za dhati kwenu waandishi wa habari kwani mmekuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha habari muhimu za maendeleo ya nchi yetu zinawafikia
watanzania kwa wakati lakini pia mimi binafsi nishukuru kwa kunipa
ushirikiano kila nilipowahitaji katika kazi za Wizara yangu na kazi yenu ni
njema. HONGERENI SANA.
2
Ndugu Waandishi wa Habari,
Nchi ya Tanzania imepata nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano
wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika
Zanzibar, tarehe 4-8 Machi, 2024. Mkutano utahudhuriwa na
wageni takriban 300 kutoka nchi 56 wanachama wa Jumuiya ya
Madola.
Mgeni rasmi katika mkutano huu anatarajiwa kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu
Hassan na atakayefunga Mkutano ni Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Aidha, Mwenyekiti wa Mkutano huu
ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais
Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar inaendelea na
maandalizi ya Mkutano huo kwa kushirikiana na Sekretarieti ya
Jumuiya ya Madola. Dhima ya Mkutano huu ni “Technology and
Innovation: How Digitization Paves the Way for
the Development of People-Centered Access to Justice”,
ambayo itwasilishwa na Tanzania na tayari maandalizi yote ya
kuandaa andiko yamekamilika. Aidha katika mkutano huo Tanzania
tunawania Tuzo mbili moja ni usajili wa watoto chini ya miaka
mitano na nyingine ni utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria
kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign.
Hafla ya ufunguzi itafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo
eneo la Airport Zanzibar.
3
Ndugu Waandishi wa Habari,
Maandalizi ya mkutano huu yanaendalea ambapo vinafanyika
vikao mbalimbali kwa njia ya mtandao kati ya Wizara zetu mbili na
Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola kwa lengo la kuratibu kwa
pamoja maandalizi ya Mkutano huo.
Aidha, Kamati Kuu ya Maandalizi inaendelea na maandalizi
ambapo tarehe 11 Januari, 2023 ilikutana na agenda ilikuwa ni
kuunda Kamati ndogo za maandalizi ya mkutano na kufahamu
majukumu ya Kamati hizo. Kikao cha pili kilifanyika tarehe 17
Januari 2024 na agenda ilikuwa ni kupokea na kujadili taarifa na
mahitaji ya bajeti. Kikao cha nne(4) kilifanyika tarehe 22 Januari
2024 na agenda lilikuwa ni kupitia na kujadili taarifa za maandalizi
ya mkutano zitakazowasilishwa kwenye kikao cha kamati ya Taifa
ya Maandalizi. Hadi hivi sasa tumeshatengeneza Roadmap ya
masuala yote kuhusu mkutano kuanzia tarehe 31/01/2024 hadi
08/03/2024.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Jumla ya Kamati ndogo za Maandalizi saba (7) zimeundwa na zina
wajumbe kutoka Wizara na taasisi mbalimbali za Serikali zote mbili.
Kamati hizo ni Kamati ya Bajeti, Ununuzi na Fedha; Kamati ya
Mapokezi, Itifaki, Usafiri na Malazi; Kamati ya Ukumbi, Mapambo,
Chakula na viburudisho, Mchapalo, zawadi, Burudani na TEHAMA;
Kamati ya Usajili, Usajili, Ulinzi na Usalama; Kamati ya Habari na
Machapisho; Kamati ya Afya; Kamati ya Nyaraka na Kamati ya
Utalii.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola imeshafanya ziara mara mbili
kushirikiana na timu ya wataalam wetu. Lengo la ziara hizo mbili ni
kutathmini kwa pamoja hali ya maandalizi ya mkutano huo,
kukutana na Kamati ndogo za Maandalizi na kutembelea maeneo
yanayohusiana na Mkutano huo ikiwemo kumbi za mkutano, hoteli
4
za malazi ya wageni na vivutio vya utalii kwa wageni watakaoshiriki
katika mkutano.
Ndugu Waandishi wa Habari
Mkutano huu sio tu utaitangaza nchi yetu katika anga za kimatifa
bali utatumika kama chazo cha mapato ya fedha za kigeni. Aidha
mkutano huu utakuwa fursa kwa wajasiriamali wadogo na wakati
kufanya baishara zao eneo la mkutano.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Kwa kumalizia hotuba yangu, naomba niwakumbushe tena kuwa
hii nafasi adhimu ambayo nchi yetu imebahatika katika mwaka huu
kuweza kuwa mwenyeki wa kikao hiki. Niwakumbushe kuwa Dunia
ina imani na Tanzania kuhusu utawala wa Sheria na Haki ndio
maana mwishoni mwa mwaka jana pia mkutano mkubwa wa 77 wa
Haki za Binadamu na Watu ulifanyika hapa Nyumbani Mkoani
Arusha. Ikumbukwe kuwa Kamisheni ya Afrika ya Haki za
Binadamu na Watu hawaendi mahali bila kujihakikishia masuala ya
amani yako vizuri, hivyo niwasihi wanahabari kuendeleza
kuzitumia kalamu zenu katika kueneza tunu ya amani na mazuri
yote ambayo Serikali yetu inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu
Hassan inayatekeleza bila kuacha kukielezea kwa kina kikao hiki
na manufaa yake kwa watanzania. Mkutano huu kufanyika nchini
kwetu unadhihirisha pasi na shaka juu ya kuaminika kwetu katika
anga la kimataifa kwani mkutano wa mwisho wa Mawaziri wa
Jumuiya ya Madola ulifanyika Mauritius mwaka 2022, sio rahisi
mkutano unaofuata kufanyika tena Afrika ila kwa kuwa Rais wetu
wa awamu ya sita ameifungua nchi, tulikubaliwa bila kupingwa
kuwa mwenyeji wa mkutano huu.
Asanteni sana!
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania na Kazi iendelee!
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇