Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mtendajiwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishiwa Umma (PSSSF).
Taarifa iliyotokewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza kwamba Badru anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo CPA Hosea Kashimba ambaye Ikulu imesema atapangiwa kazi nyingine.
Pia Rais amemteua Dk. Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuchukua nafasi ya Badru. "Uteuzi huu ulianza tarehe 06 Februari, 2024", taarifa imesema.
Katika taarifa imeelezwa pia kuwa Rais amemteua pia aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Mazingira (Biodiversity Conservation) Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kuchukua nafasi ya Dk. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake na uteuzi huo ulianza tarehe 03 Februari, 2024.
Your Ad Spot
Feb 7, 2024
RAIS DK. SAMIA ABADILISHA MKURUGENZI MKUU MFUKO WA PSSSF
Tags
featured#
Uchumi#
Share This
About Bashir Nkoromo
Uchumi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇