Na Bashir Nkoromo,CCM Blog, Dar es Salaam
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza maziko ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa yanayotarajiwa kufanyika Wilayani Monduli Mkoani Arusha Jumamosi Februari 17, 2024.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitangaza ratiba ya mazishi ya kiongozi huyo, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Oysterbay, Dar es Salaam, leo Jumapilii, Februari 11, 2024,
Amesema katika kipindi cha siku tano za maombolezo yaliyotangazwa na rais Dk. Samia jana, Taifa litaendelea na shughuli za umma na kijamii sanjari na kushirikiana na wanafamilia katika ratiba ya msiba kama ilivyoandaliwa na kamati ya mazishi ya Kitaifa na wanafamilia.
Waziri Mkuu, amesema kabla ya mazishi hayo mwili wa Hayati Lowassa unatarajiwa kuagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Jumanne Februari 13, 2024, na Jumatano Februari 14 mwili wa Hayari Lowasa utafanyiwa ibada takatifu na kuuaga katika Kanisa la KKKT Azania Front na Alhamisi Februari 15 mwili utasafirishwa hadi jijini Arusha ambako viongozi na wananchi watapa fursa ya kuaga katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Lowassa amefarikii jana Jumamosi, Februari 10, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu, na tangazo la kifo lilitolewa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, baada ya Waziri Mkuu huyo mstafu kufariki dunia saa 8 mchana.
Your Ad Spot
Feb 11, 2024
Home
featured
Kitaifa
RAIS DK. SAMIA KUONGOZA MAZIKO YA LOWASSA MONDULI J'MOSI FEB 17, MWILI KUAGWA DAR ES SALAAM J'NNE FEB13, JIJINI ARUSHA ALHAMISI FEB 15
RAIS DK. SAMIA KUONGOZA MAZIKO YA LOWASSA MONDULI J'MOSI FEB 17, MWILI KUAGWA DAR ES SALAAM J'NNE FEB13, JIJINI ARUSHA ALHAMISI FEB 15
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇