Masasi, Mtwara
Msafara wa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda umepata ajali katika kijiji cha Sululu, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara leo saa 9 alasiri ikihusisha zaidi ya magari 10 yaliyokuwepo katika msafara huo.
Msafara huo ulikuwa ukirejea jijini Dar es Salaam, baada ya ziara kusitishwa kutokana na kifo cha Waziri Mstaafu Edward Lowasa kilichotokea jana.
Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu wasiopungua 7 wamejeruhiwa na kupelekwa hospital ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara na huku kukiwa hakuna kifo chochote. Hali ya Makonda ni salama.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇