Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Namibia Marehemu Dkt. Hage Geingob katika uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024. Hayati Rais Geingob alifariki dunia tarehe 04 Februari na anatarajiwa kuzikwa tarehe 25 Februari, 2024 katika Makaburi ya Mashujaa ya Heroes’ Acre Jijini Windhoek.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu Monica Geingos mara baada ya kuzungumza na kutoa heshima za mwisho katika mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Namibia Marehemu Dkt. Hage Geingob kwenye uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Rais wa Namibia Dkt. Nangolo Mbumba mara baada ya kuzungumza na kutoa heshima za mwisho katika mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Namibia Marehemu Dkt. Hage Geingob kwenye uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mazishi ya
Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Namibia Marehemu Dkt. Hage Geingob kwenye
uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024.
Hayati Rais Geingob alifariki dunia tarehe 04 Februari na anatarajiwa
kuzikwa tarehe 25 Februari, 2024 katika Makaburi ya Mashujaa ya Heroes’
Acre Jijini Windhoek.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇