Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilombero, Hemed Msuya, akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya CCM kata ya Msolwa Stesheni, Wilayani Kilombero, mkoa wa Morogoro.
NA VICTOR MAKINDA, KILOMBERO - MOROGORO.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Kilombero, wametakiwa kuisimamia
serikali ili iendelee kutekeza ilani ya uchaguzi ya chama hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero mji, wilaya ya Kilombero, Kasim Nakapala akizungumza katika maadhimisho ya miaka 47 ya C
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Wilaya ya Kilombero, Hemed Msuya,
wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika
kwa ngazi ya wilaya Kata ya Msolwa
Steheni, Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro jana.
Msuya amesema kuwa CCM ndiyo chama kilichopata ridhaa ya
wananchi ya kuunda serikali kupitia sanduku la kura, hivyo viongozi wa chama
hicho wana dhima ya kuwasimamia
watendaji wa serikali na kuwawajibisha viongozi wote wanaoendekeza urasimu na
ugoi goi katika kuwahudumia wananchi.
“Msiogope, chama ni
zaidi ya serikari, kipo juu na serikali ipo chini ya chama. Mjitambue kuwa
ninyi ni wasimamizi wa kuwasimamia viongozi wa serikali ili wafanye kazi kwa
bidiii kutekeleza ilani ya CCM,” alisema Msuya.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM, Wilaya ya Kilombero, akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya chama hicho.
Aliongeza kusema kuwa CCM
wilayani Kilombero, haitasita kuwachukulia hatua watendaji wa serikali
wasiotimiza wajibu wao wa kuwahudumia
wananchi.
Akizungumza kuhusu miaka 47 tangu kuzaliwa kwa CCM, Msuya amesema
kuwa chama hicho kinajivuni misingi iliyoasisi na kuilinda, ikiwa ni uzalendo,
utu, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Baadhi ya wanachama wa CCM walohudhuria sherehe hizo
Naye Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Ifakara Mji, wilaya ya Kilombero, Kasim Nakapala, akizungumza kwenye
maazimisho hayo, alisema kuwa wakati tunasherehekea miaka 47 ya CCM, Halmashauri ya Kilombero imepokea miradi
mingi ya maendeleo hivyo ni wajibu wa watendaji wote wa serikali kusimamia
miradi hiyo ili ilete tija kwa wananchi.
Viongozi wa wilaya wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho hayo.
“Tunaimshukuru serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kutuletea
miradi mingi ya maendeleo wilayani kilombero, ikiwa ni miradi ya elimu,
afya,kilimo, umeme na ujenzi wa barabara, hivyo watendaji wa serikali wanapaswa
kuendana na kasi ya rais katika kusimamia miradi hiyo ili ituletee maendeleo," alisema Nakapala.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇