Na Hemed Munga, Iramba.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida Lucy Shee, amewahimiza Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Old Kiomboi na Wajumbe wa Kamati ya Siasa wa CCM wilayani Iramba kushiriki kikamilifu tena kwa uadilifu katika malezi ya watoto kwa sababu viongozi wazuri wanatoka katika familia iliyolelewa vizuri.
Akizungumza katika mafunzo ya wajumbe hao yaliofanyika wilayani hapa juzi, Katibu Shee alisema viongozi wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na watoto na jamii kwa jumla kwa kuwa na tabia nzuri katika vitendo, kauli zao na waaminifu.
Amewataka kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia wajibu wao, haki na mipaka yao.
Pia, amesema wanatakiwa kua na tabia ya kukubali kujifunza hata kwa mtu mdogo kwao kwa sababu huenda anajua zaidi na mdogo kujifunza kwa mkubwa huenda akawa anafahamu zaidi yake.
"Lazima tukubali kujifunza wakati wote na tujifunze bila ya kikomo," alisisitiza.
Kwa upabde wake Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani wa Singida Elphas Lwanji aliwamewataka viongozi hao, kufanya kazi kwa mujibu wa katiba na miongozo iliyowekwa na chama hicho.
Aliwakumbusha viongozi hao kuendelea kuhakikisha uhai wa Chama unadumu kwa kuingiza wanachama wapya ambao wamesajiliwa kwa mfumo wa kielektroniki.
Aidha, amewasisitiza kufanya vikao vya kikanuni, kusikiliza kero na kutaja mafanikio yaliotekelezwa kupitia ilani ya Chama hicho ya mwaka 2020 hadi 2025.
"Ndugu zangu, Old Kiomboi ni moja ya kata ambayo mmeletewa miradi mingi na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hivyo kuweni mstari wa mbele kupigia debe yaliotekelezwa na Rais wetu," amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman Mwenda amewakumbusha falsafa ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya kuwataka viongozi kutenda yale ambayo wanayatarajia kuyaona watu wanaowaongoza.
Aidha, amewahusia kuendelea kuitunza heshima ya Chama na kutoonekana katika maeneo ambayo yanadaiwa kutokua ya maadili kwa viongozi.
"Niwahusie kuziishi imani za Chama Cha Mapindunzi kwa sababu kinaheshima kubwa ndani ya nchi, Afrika na duniani
Na sisi wengine hatukotayari kuona heshima ya chama chetu inavurugwa kwa sababu yako wewe, tutakua wakali, kulinda chama chetu, hadhi na heshima ya viongozi," amesisitiza.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM tawi la Meli katika kata hiyo Elieze Msolomon, alipongeza viongozi hao kwa sababu ya tabia ya kukumbushana mara kwa mara, hivyo wanafahamu kinachokuja mbele yao na kuahidi kufanya kazi ipasavyo.
Mafunzo hayo yamefanyika ikiwa ni siku moja baada ya kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM na kutimiza miaka 47, ikiwa ni sehemu ya kuendelea kutekeleza maazimio kutoka Makao Makuu ya CCM.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, Lucy Shee akiwaasa wajumbe wa Halmashauri kuu ya kata ya Old kiomboi na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Iramba mkoani humo, wakati wa semina elekezi iliyofanyika katika kata hiyo wilayani hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Mwenda, akizungumza wakati wa semina elekezi iliyofanyika katika kata Old kiomboi wilayani hapa.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kulia, Iddi Kijamba akiwa na badhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Old kiomboi wakifuatilia mafunzo toka kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, Lucy Shee, leo wakati wa semina elekezi iliyofanyika katika kata hiyo wilayani hapa. (Picha zote na Hemedi Munga)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇