LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 8, 2024

WABUNGE WATOA MAONI BENKI YA DUNIA

Mtandao wa Wabunge Duniani kuhusu Masuala ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (Tawi la Tanzania) wamekutana na Benki ya Dunia kwa lengo la kutoa maoni katika Mradi wa Maendeleo wa Tanzania wa Benki ya Dunia unaokamilika sasa na kutoa Mapendekezo kwa Mradi unaotarajiwa kuanza 2025 hadi 2029. 

Jumla ya Wabunge 35 wameshiriki Mkutano huu wakiwemo Wenyeviti wa Kamati za Bunge 12 na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge Duniani kuhusu Masuala ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani ni Mhe Neema Lugangira, na Mgeni Rasmi alikuwa Mhe Daniel Sillo ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti lakini pia ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao huu. 

Aidha, Benki ya Dunia wamepokea maoni na Mapendekezo ya Wabunge na kuahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na Tawi la Mtandao wa Wabunge Duniani kuhusu Masuala ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani.






 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages