LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 5, 2024

DK. MWINYI AFANYA KIKAO CHA NA SEKRETARIETI YA KAMATI MAALUM NA SEKRETARIETI ZA CCM MIKOA NA WILAYA ZANZIBAR

Zanzibar, leo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amefanya kikao cha kwanza na Sekretarieti ya Kamati Maalum, Sekretarieti  za Mikoa na Wilaya CCM Zanzibar, kikiwa cha kwanza na Watendaji hao.

Katika kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Afisi kuu CCM Kisiwandui leo Februari 5, 2024, Makamu Mwenyekiti Dk. Mwinyi amewasisitizia kwamba kazi kuu ya Chama cha siasa ni kushinda chaguzi za dola.

Dk. Mwinyi amempongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kusimamia vema Chama Cha Mapinduzi na kukiimarisha na kuwapongeza watendaji kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuimarisha chama na kutekeleza majukumu yao ya  kila siku.

Kuhusu Chaguzi,  Makamu Mwenyekiti Dk. Mwinyi amewataka watendaji kutoa fursa sawa kwa wagombea wote na kujiepusha kutengeneza makundi wakati wa uchaguzi, huku akiwasisitiza watendaji hao kuwa wana wajibu wa kusimamia kanuni za chama kuhakikisha umoja, amani na utulivu una kuwepo ndani ya chama.

Amewataka wana CCM wote kuwa mstari wa mbele kuelezea vema mafanikio ya ilani ya utekelezaji wa CCM kwa kazi nzuri  iliyofanyika kwa kugusa sekta nyingi za utekelezaji pamoja na kuvuka lengo ikiwemo sekta elimu, afya , barabara, maji na uwezeshaji wa vikundi vya wajasiriamali.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza kikao hicho.
Kikao hicho kikiendelea kwa wajumbe kutoa maoni.
Mjumbe akitoa maoni kwenye kikao hicho.
Mjumbe akitoa maoni kwenye kikao hicho.
Mjumbe akitoa maoni kwenye kikao hicho.
Mjumbe akitoa maoni kwenye kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages