LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 23, 2024

WAJASIRIAMALI WANAWAKE WAOMBA KUWEZESHWA KUMUDU SOKO LA AFRIKA

Katibu tawala Msaidizi upande wa biashara, viwanda na uwekezaji mkoani Morogoro  Beatrice Njawa akizungumza katika mafunzo ya ujasiriamali ya wanawake yanayoendeshwa na Chemba ya Biashara anzania (TWCC) mjini Morogoro jana. 


NA VICTOR MAKINDA.MOROGORO

Wajariamali wanawake mkoani Morogoro wamewaomba wadau wa ukuzaji wa biashara kutoishia mijini na kufika kwenye vijijini kutoa elimu na usaidizi wa ukuzaji biashara ili kuwajengea uwezo kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika na zinazoweza  kukabili ushindani wa soko ya ndani na nje ya nchi.


Wajasiriamali hao waliyasema hayo jana wakati wakiongea kwenye mafunzo ya wajasiriamali wanawake kuhusu kanuni, taratibu na sheria za kufanyabiashara kwenye soko la Afrika (AICFTA) yaliyoandaliwa na Chemba ya wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC) ulifanyika mjini hapa.


Mmoja wa wajasiriamali hao Eva Kipalile mkazi wa Kijiji cha Mbingu kata ya Igima Wilayani Mlimba alisema, licha ya kuzalisha vikapu, ungo na mazao aina ya Kakao lakini wanakabiliwa na changamoto ya kukosa masoko ya nje kutokana na kukosa nembo ya kuhakiki ubora (TBS), Misimbomilia(Barcods) na usajili wa urasimishaji biashara kutoka BRELA.


“watu hao wanapaswa kufika vijijini kwetu na wasibaki mjini, sababu leo tumejifunza vitu vingi, wenzetu wanaweza kutoka kwenda kufanya biashara na mataifa mbalimbali lakini sisi tunashindwa kutoka sababu hatuna vitu ambavyo ni muhimu na tumevijulia hapa” alisema Kipalile.



Naye Makamu Mwenyekiti wa TWCC Taifa Rose Romanus alisema ajenda yao ni kuhakikisha wanawake wanamiliki pesa kwa kutimiza malengo waliyojiwekea kwa kulifikia soko huru la Afrika.


Akifungua mafunzo hayo Katibu tawala Msaidizi upande wa biashara, viwanda na uwekezaji mkoani hapa Beatrice Njawa aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuzalisha bidhaa zenye ubora zinazokidhi viwango vya masoko likiwemo soko huria la Afrika linalohudumia nchi 54.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages