Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Mary Chatanda akihutubia wakati wa kufunga semina Kikundi cha Wabunge Vinara Wanawake katika Siasa iliyofanyika jijini Dodoma ambapo walijadili namna ya kwenda kuongeza ushiriki na uwakilishi wa wanawake katika uongozi na siasa kupitia miswada mitatu inayopelekwa bungeni. Mwenyekiti wa kikundi hicho ni Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira.
WABUNGE wanawake wametakiwa kumtua mzigo begani Rais Samia Suluhu Hassani kuhusu uwepo wa sheria sahihi inayojali usawa wa kijinsia katika uongozi mbalimbali.
Msisitizo huo umetolewa na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Chama Mapinduzi CCM, Halima Mamuya na Mary Chatanda wakati wa semina ya Kikundi cha Wabunge Vinara Wanawake katika Siasa iliyofanyika jijini Dodoma ambapo walijadili namna ya kwenda kuongeza ushiriki na uwakilishi wa wanawake katika uongozi na siasa kupitia miswada mitatu inayopelekwa bungeni.
Chatanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), amesema kuwa wakati wa Mungu wa kuwapigania wanawake ni sasa kwa kumuunga mkono Rais Samia ambaye ni namba moja kwa kupigania suala la usawa wa kijinsia.
Naye Mamuya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa UWT, amesema kuwa wabunge wanawake na viongozi wengine kupambania usawa wa kijinsia siyo ombi bali ni lazima tuhakikishe tunamtua mzigo begani Rais Samia.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba, Sheria, Florence Kyombo akiwa na Chatanda.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Halima Mumuya akitoa nasaha zake wakati wa semina hiyo.
Wabunge vinara wakiwa katika picha na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Chatanda na Mumuya.
Chatanda akiwa na wabunge vinara wanaume
Mwenyekiti wa Kikundi cha wabunge vinara, Neema Lugamgira
Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Esther Matiku akitoa maoni yake wakati wa semina
Mbunge wa Mbarali (CCM), Bahati Ndingo
Mbunge wa Viti Maalumu na Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake bungeni, Shally Raymond
Lugangira akielezea lengo la semina hiyo
Mbunge kinara mwanaume, ambaye ni Mbunge wa Lupembe, Edwin Swale
Mjumbe wa KIkundi hico, ambaye pia ni Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda
Mjumbe wa Kikundi hicho, Mohamed Mwinyi.
Mjumbe wa kikundi hicho, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ng'wasi Kamani,
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇