Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM
Katika kuhakikisha uelewa wa mtaala ulioboreshwa 2023 unajikita vema kwa walengwa wote nchini, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imeandaa mafunzo mengine ya siku mbili kwa Walimu kutoka shule zisizo za serikali wa Kidato cha Kwanza Mkondo wa Elimu ya Amali, yatakayofanyika katika Chuo cha Ualimu Morogoro, kuanzia kesho Jumatatu, Januari 8, 2024.
Taarifa ya mwaliko iliyotolewa na Murugenzi Mkuu wa TET Dk. Aneth Komba, kwa washiriki imeeleza kuwa mafunzo hayo yatafanyika katika Chuo hicho maarufu, Januari 8 hadi 9, 2024, na washiriki wote wanatakiwa kuwa ukumbini kuanzia saa 2: asubuhi.
"Tafadhali zingatia kuwa walimu wanaoalikwa ni wa Kidato cha Kwanza tu hivyo, shule zote za sekondari sisizo za Serikali zilizoidhinishwa kufundisha masomo ya Amali ziwasilishe walimu wanne (04) wanaofundisha masomo ya taaluma ya Hisabati, Elimu ya Biashara (Business Studies), Kiingereza na Historia ya Tanzania na Maadili (mwalimu mmoja kwa kila somo)", amefafanua Dk. Aneth katika mialiko hiyo.
Dk. Aneth ameomba kila mshiriki kufika na tableti au kompyuta atakayotumia wakati wa mafunzo na kwamba TET itagharimia wawezeshaji, ukumbi pamoja na chakula wakati wa mafunzo kwa washiriki wote na Taasisi zinazomiliki shule au shule husika zinaombwa kugharamia malazi na usafiri.
"Orodha ya shule imeambatishwa kama ilivyoletwa kwako kwa barua ya Kamishna wa Elimu yenye Kumb. Na. CA.229/238/01/32 ya tarehe 29/12/2023. Tafadhali katika
orodha iliyoambatishwa zingatia idadi ya walimu waliotajwa katika barua hii kwa kila somo", ameeleza Dk. Aneth na kushuuru kila mmoja kwa ushirikiano.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)
Dk. Aneth Komba, akieleza muktadha na maudhui ya Mitaala iliyoboreshwa 2023, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
Mitaala hiyo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi -Elimu wa mikoa na maafisa
elimu ya Msingi wa Halmashauri nchini kote, iliyofanyika katika Ukumbi
wa Shule ya Msingi Bernard Bendel, Kola B Mjini Morogoro, Janauari
03, 2024. (Picha na Maktaba ya Blog ya Taifa ya CCM)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇