Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Morogoro
Wakati Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk. Frankilin Rwezimula, akisema busara na hekima za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ndizo zilizomewezesha kufanyika mageuzi makubwa ya sera ya Elimu nchini, na kuibua Mitaala iliyoboreshwa, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dk. Aneth Komba, amesema somo jipya la Historia ya Tanzania na Maadili limebeba maudhui yanayolenga kumjenga Mtanzania kuwa mzalendo na muwajibikaji anayefahamu historia, desturi, mila na maadili ya nchi yake.
Dk. Rwezimula na Dk. Aneth wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakizungumza ya katika ufunguzi wa mafunzo ya mitaala iliyoboshwa yaliyokuwa mahususi kwa Walimu wa shule za sekondari za serikali na zisizo za serikali ambazo zinatekeleza mtaala wa sekondari mkondo wa Amali, katika awamu ya kwanza, yaliyofunguliwa na Dk. Rwezimula katika Chuo cha Ualimu, Morogoro, leo Januari 8, 2024.
HOTUBA YA DK. ANETH IKIFAFANUA KUHUSU MTAALA ULIOBOESHWA HII👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇