JNICC Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Andulrahman Kinana amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi huku akiahidi CCM kuwapa fursa kwa kuwapitisha akisema wanao uwezo wa kuongoza.
Kinana amesema hayo katika Mkutano Mkuu Maalumu wa kupokea wananchama wapya 1,167 wa Seneti ya Vyuo Vikuu wa DIT, CBE, IFM na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kutoka tawi la Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki, uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, leo.
Amesema, CCM inawategemea vijana kwa ushauri, kujenga hoja na kukosoa, hivyo watambue wao ni watu wa kisasa, wasomi na wanakwenda na kasi ya upatikanaji wa taarifa hususan kupitia mitandao ya kijamii, hivyo wanayo chachu ya mawazo kwa Chama na wasifikiri kuna sehemu nyingine mawazo yatatoka bali ila kwao kwa wao ni taifa la leo.
"Kutokana na hilo mnao uwezo mkubwa wa kutushauri, kutujenga na kutukosoa, tunakutegemeeni sana, toeni mawazo. mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mitaa, nawasihi vijana jitokezeni na gombeeni katika nafasi zote," alisema.
Kinana alisema Chama kitafanya kila linalowezekena kuwapitisha vijana wengi katika nafasi za kugombea kwani yeye na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan watafanya kila jitihada kuwapitisha vijana wengi.
"Nawasihi nendeni mkagombee nafasi zote na Chama tutatoa maelekezo kufanya linalowezekena kuhakikisha vijana wanapewa nafasi nanyi hakikisheni mnakipa ushindi Chama chenu," alisema.
Kinana alisema CCM ni kubwa, hivyo wanapaswa kukilinda, kujipanga, kuweka mikakati na kugawa majukumu.
Alisema yapo mambo yanayochangia kukipa ushindi Chama ukiwemo utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, hivyo aliwataka vijana kuchagua viongozi wenye uwezo na sio wa kubebwa wala kutumia fedha kupata nafasi.
Hata hivyo, alisema Chama kisingependa kupata malalamiko bali kitachagua viongozi kulingana na sifa zao.
Kinana aliahidi kutoa kompyuta, mashine ya kuchapisha na ‘printa’ kwa vijana hao wajitegemee katika seneti yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abas Mtemvu alisema ofisi ya Chama mkoa itachamgia sh. milioni mbili katika mfuko wa vijana zitakazosaidia kununua vifaa mbalimbali ambavyo vitawawezesha kujitegemea.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana, akizungumza na Viongozi na Wanachama katika Mkutano wa Ukaribisho wa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi za CCM kwa Wanachama 1170 wa Matawi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu katika Vyuo Vya CBE,DIT,IAE patika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Mkoa wa Dar Es Salaam.Wanachama Wapya wakila Kiapo Cha Chama. (Picha na Fahadi Siraji wa CCM)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇