LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 28, 2024

JAJI DK. FELESHI AFURAHISHWA NA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Dkt Eliezer Feleshi  akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu, na Huduma za Ushauri, Haruni Matagane kuhusu utendaji wa ofisi hiyo alipotembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Maadhimisho ya  Wiki ya Sheria kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma Januari 28, 2024. 

Jaji Dkt Feleshi ambaye ameonesha kufurahishwa na maonesho hayo, amehimiza uchapakazi, uadilifu, kusikiliza vyema changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

 Aidha, Dkt.Feleshi amesema kuwa wana mpango wa kuanzisha kituo cha pamoja cha taasisi za sheria ili kupanua wigo wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi haraka. 

Jaji Dkt Feleshi akimsikiliza kwa makini mmoja wa wananchi aliyefika Banda la Wakili Mkuuu wa Serikali kutoa malalamiko yake ya kudhulumiwa haki yake.
Mmoja wa wananchi (aliyekaa kushoto) akipata maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Jaji Dkt. Feleshi akisikiliza kwa makini wakati Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Nicodemus Mushi akitoa maelezo kuhusu utendaji wa mamlaka hiyo.


Jaji Dkt Feleshi akisalimiana na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha alipowasili kwenye maonesho hayo.
Akitembelea maonesho hayo


Banda la Tume ya Utumishi wa Mahakama

Tume ya Usuluhishi na Uamuzi
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba
Shule Kuu ya Sheria Chuo Kikuu cha Dodoma


Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Jaji Dkt. Feleshi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama Tanzania, Beatrice Patrick.

Jaji Dkt Feleshi akiagana na baadhi ya viongozi wa mahakama baada ya kumaliza kutembelea maonesho hayo yatakayofikia kilele Februari Mosi, 2024 kwenye viwanja vya Chinangali Park ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages