LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 28, 2024

BUSARA ZA YAHYA MSANGI: CHADEMA BORA WANGEENDA MAKAO MAKUU YA CCM, KULIKO WALIVYOENDA OFISI ZA UN

Juzi juzi, Chadema walifanya maandamano na kwenda kuyatua Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN), jijini Dar es Salaam. Chadema wenyewe walidai kilichowapeleka ofisi za UN ni kuwasilisha malalamiko yao makuu ambayo wanasema ni Katiba, Tume ya Uchaguzi na gharama ya maisha kuwa juu.

Kuna mdau mmoja Yahya Msangi, Mtanzania anayeishi nchini Togo, ambaye hufuatilia kwa karibu mambo mbalimbali yakiwemo ya siasa, inaonekana alifuatilia hata hayo maandamano, kisha akaandika kwenye ukurasa wake wa Facebook mambo ambayo nadhani yananoga kuwafikia wengi.

"Nisingependa kujadili kama kweli Katiba, Tume na gharama za maisha ni shida. Kila mtu ana mtizamo wake. Ila ningependa kujadili je, Ofisi za UN ndio ilikuwa sehemu sahihi kulalamika?

Nadhani kuna watu hawajui UN ni nini? Au wamedanganyana kudhani UN ina Mamlaka juu ya nchi huru (sovereign state). Nimeona hata Jenerali Ulimwengu amewakosoa!

Niwakumbushe tu jirani zetu DRC wanawafukuza Wanajeshi wa UN. Tena Kwa kuwashambukia. Na UN imeamua kuondosha askari wake (blue hats). Hawatakiwi na raia. Ingekuwa UN ina mamlaka juu ya DRC isingeondoka. UN inajua haina hayo mamlaka.

Viongozi wa Chadema sijui ni kukosa uwezooo au udanganyifuu? UN haiwezi kuiamuru Tanzania ibadili Katiba, Tume au ipunguze bei ya mchele!

Hivi hawajui Katiba ya UN ina mapungufu na nchi nyingi inataka irekebishwe? Iweje nchi 5 tu ziwe Baraza la Usalama na wengine wazuiwe? Unapeleka kesi ya kuibiwa jogoo kwa jambazi wa magari?

Viongozi wa Chadema wamewahi kusoma Charter iliyoundwa UN? Inasema hivi kuhusu nchi wanachama "wanachama wa UN ni nchi huru zenye maamuzi na madaraka kamili yasiyoweza kuingiliwa na UN wala mwanachama wa UN".  Leo chadema mnataka UN iamue bei ya sembe? Hebu tuambieni toka uhuru UN imewahi kuiagiza serikali ifanye nini?

Si UN ingeingia Kenya wakati kina Odinga, Kalonzo, Wajakoya na Martha wakivaa sufuria kichwani?

Sasa kwenye kikosi kazi mnafuata nini kama mnashitaki Ofisi ya UN? Mkiambiwa tokeni mkachukue majibu UN? Yaani sawa una ugomvi na kakaako na unahudhuria vikao vya familia lakini ukitoka hapo unaenda kwa mganga Sumbawanga umuombe ampige kakaako radi ya utosi!

Si mlishatuambia mumeshitaki serikali EU na The Hague? Mlipata nini? Si mlienda Mahakama ya Afrika Mashariki na ya Afrika ? Mlipata nini? Sasa mtaenda mara ngapi ofisi za UN kwa maandamano?

Si mnadai mna nguvu ya umma? Kwa Nini hamuitumii kama kweli mnayo?

Hebu acheni ushamba. Safari ijayo nawashauri mpeleke malalamiko yenu Ofisi Kuu ya CCM Dodoma au hata vijiweni. Itafaa kuliko kwenda ofisi za UN. Mkumbuke hizo mnazoita "haki" zimeorodheshwa kwenye UN DECLARATION OF HUMAN RIGHTS OF 1948. Hakuna haki ya mchele buku, Katiba wala tume huru. UN iliachia nchi zijiamulie zenyewe. Mnataka mchele bure, tume ya babaako au katiba yenye kurasa moja ni hiari ya nchi.

Chadema maziwa huwezi kuyapata mtoni. Utatakiwa ufuge! MFANO HAI: ISRAEL IMEKAIDI MAAGIZO YA UN. NA UN IMEKOSA CHA KUWAFANYA

Chadema Wakiandamana kwenda UN
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages