LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 20, 2024

DKT NCHIMBI: WANACCM TUUNGANE TUSIKUBALI KUYUMBISHWA


 *Nchimbi; CCM itadumisha Mapinduzi, Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar*


Kuhusu msimamo wa CCM kudumisha dhamira ya waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na kuimarisha umoja, utulivu na amani ya Wazanzibar, Katibu Mkuu Ndugu Nchimbi amesisitiza kuwa lazima wanaCCM waungane na wasikubali kuyumbishwa katika suala hilo, akitoa wito kwa Chama cha ACT Wazalendo, ambacho kiko katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, kuwa tayari kuzungumza linapotokea jambo lolote la kujadili.


“Mmenipeleka kwenye kaburi la muasisi Abeid Aman Karume na kila kiongozi anapokabidhiwa ofisi ya kitaifa anapokuja hapa Afisi Kuu kwa mara ya kwanza lazima apelekwe kufanya dua kwenye kaburi la mwasisi wetu na walioweka utaratibu huu hawakutaka tuishie kufanya dua pekee walimaanisha kutukumbusha kwamba Chama hiki ni cha kimapinduzi. Serikali yetu ni Serikali ya Kimapinduzi ni Serikali iliyopatikana kwa maamuzi ya ASP kutaka kuikomboa nchi yetu kuwarudishia walio wengi madaraka waongoze nchi yao wajitafutie maendeleo. 


“Ukiona mtu ana hamu hamu hivi ya kuona Serikali ya Umoja huu imevunjika ujue muda wote anapotembea pua zake zinatamani damu za watu kwa hiyo lazima tuungane tushirikiane wana CCM wote msimamo wetu uwe mmoja tusiyumbishwe. Tunawapa shime wenzetu wa ACT-Wazalendo kwamba wajue nao wana wajibu wa kuunga mkono Serikali ya Umoja wa kitaifa na kama kuna mambo madogo madogo tuzungumze,” amesema Ndugu Nchimbi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages