LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 20, 2024

DKT NCHIMBI AAHIDI KUWATUMIKIA WATANZANIA KWA UADILIFU MKUBWA



Ndugu Nchimbi amewahakikishia wanaCCM na wananchi kwa ujumla kuwa katika kipindi ambacho atakuwa Katibu Mkuu wa CCM, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameahidi kuwatumikia watanzania kwa uadilifu mkubwa, Chama kitaimarisha usimamizi wa Serikali zake zote mbili, ili kuhakikisha zinatimiza wajibu wa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 – 2025. 


“Kazi anayofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar ni kubwa, inahitaji tu wana CCM kupitia chama chao kuimarisha usimamizi wa Serikali hizi. Ninawakikishieni tutazisimamia Serikali hizi, chini ya Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi,” amesema Ndugu Nchimbi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages