LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 25, 2024

DK NCHIMBI: CCM ITASHINDA KWA KISHINDO CHAGUZI ZIJAZO

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dk. Emmanuel John Nchimbi, akitoa hotuba ya ufunguzi, kufungua kikao cha kazi cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambao wanakutana katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJLNS), Kibaha, mkoani Pwani. Pamoja na Komredi Nchimbi, viongozi wengine waliokutana katika kikao hicho kujadili agenda mbalimbali ni pamoja na Komredi Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia, Komredi Obert Moses Mpofu, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU- PF cha Zimbabwe, Komredi Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini, Komredi Francisco Mucanheia, ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO cha Msumbiji, Komredi Manuel Domingos Augusto, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA nchini Angola (wa pili kushoto) na (mwenye suti nyeusi) (picha na Scolastica Msewa).


 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dk. Emmanuel John Nchimbi akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kazi cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Makatibu Wakuu hao ambao wamekutana Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), iliyopo Kibaha, mkoani Pwani, leo Alhamis Januari 25, 2024, kujadili masuala mbalimbali, ni kutoka vyama vya SWAPO (Namibia), ZANU-PF (Zimbabwe), ANC (Afrika Kusini), MPLA (Angola) na FRELIMO (Msumbiji).




Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja, wakati walipokutana kwa ajili ya kikao cha kazi, kujadili agenda mbalimbali katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) iliyopo Kibaha, mkoani Pwani. Kutoka kulia ni Komredi Obert Moses Mpofu, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU- PF (Zimbabwe), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM (mwenye shati ya kijani), Komredi Sophia Shaningwa Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia), Komredi Francisco Mucanheia ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Komredi Manuel Domingos Augusto, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa MPLA (Angola) na mwishoni kushoto ni Komredi Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini)







Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Balozi Dk.  Emanuel Nchimbi   amewahakikishia Makatibu Wakuu wa Vyama Sita vya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika kwamba Chama Cha  Mapinduzi  kina uhakika wa  kushinda kwa kishindo katika chaguzi za mwaka huu na mwaka kesho, kwa maana ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025. 

Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo  wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita vya Ukombozi  wa Nchi za Kusini mwa Afrika kilichofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kuwapongeza Chama Cha ZANU - PF cha Zimbabwe Kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi  wao walioufanya  huku akivitakia pia heri  ya ushindi  NAMIBIA NA AFRIKA KUSINI  kwenye uchaguzi wao mkuu ambao wao  wanaufanya baadae mwaka huu na ANC cha Afrika kusini ambacho kimesheherekea kumbukumbu ya miaka 112 tangu kuanzishwa kwake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages