LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 5, 2024

CHATANDA AWASILISHA MAPENDEKEZO YA UWT MSWAADA WA SHERIA YA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda akisoma mapendekezo ya UWT kuhusu mabadiliko ya sheria ya uchaguzi na siasa katika mkutano wa kukusanya maoni kuhusu mswaada huo jijini Dar es Salaam Januari 4, 2024.

WASILISHO LA MWENYEKITI WA UWT TAIFA MARY CHATANDA KUHUSU MAPENDEKEZO YA UWT KATIKA MISWAADA YA SHERIA ZA UCHAGUZI NA SIASA- JANUARI 2024 -

 HALI YA UWAKILISHI WA WANAWAKE KATIKA SIASA

 1. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019  Wenyeviti wa Vijiji 11,915 = Wanawake 246 = 2.1% Wenyeviti wa Serikali za Mitaa 4,171 = Wanawake 528 = 12.6% Wenyeviti wa Vitongoji 58,441 = Wanawake 4,171 = 6.7%2. 

Uchaguzi Mkuu 2020  Majimbo 268 = Wanawake 26 = 9.1%  Viti Maalum = 113  Wabunge wote 393 = Wanawake 143 = 37% 

MSWAADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA 

Kifungu cha 13, Kifungu kidogo 10 (C) Ili Msajili wa Vyama Vya Siasa awe na Meno, Mapendekezo ya UWT katikaKifunguhiki:  Sheria itamke wazi kwamba katika Uteuzi wa Wagombea katika Chaguzi zaNdani ya Chama na Nje ya Chama kila Chama kitateua angalua asilimia20%ya Wagombea Wanawake kwenda katika Majimbo, Kata, Serikali zaMitaana pia kwa Chaguzi za Ndani ya Vyama Vya Siasa. 

 Sheria iweke wazi muundo wa Dawati la Kijinsia, litakuwa chini yanani nalitaunganishwa vipi na Msajili wa Vyama Vya Siasa?  Sheria itamke kuwa Kila Chama Cha Siasa kitatumia asilimia Fulani yaRuzuku katika kuwajengea uwezo wanawake na makundi maalumkuwezakushiriki katika Chaguzi

 MSWAADA WA SHERIA YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI Kifungu cha 5, Kifungu kidogo cha 3 pamoja na Kifungu cha 10, Kifungukidogocha 1  Katika Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume yaTaifayaUchaguzi, Sheria itamke wazi kuwa Mwenyekiti wa Tume akiwawajinsiamoja basi Makamu Mwenyekiti wa Tume atakuwa wa jinsia ingineKifungu cha 7, Kifungu kidogo 2 (d):  Wajumbe wengine watano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wachaguliwe kwa kuzingatia jinsia na itamke badala ya kuiacha iwe tu kwa sifa nyingine ambayo Kamati ya Usaili itaona inafaa.

 Kifungu cha 9, Kifungu kidogo (2):  Wajumbe wa Kamati ya Usaili watakuwa 5 na 4 wanaingia kwa nafasi zaona1 ndio anateuliwa na Mhe Rais kwa kuzingatia jinsia lakini UWTtunapendekeza iongezwe nafasi 1 ambayo pia izingatie jinsia ili kuongezauwiano wa kijinsia katika Kamati ya Usaili Ibara Mpya katika Mswaada: 

 Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi itamke Tume yenyewe pia kuwanaSeraya Jinsia na Ujumuishwaji wa Makundi Maalum katika Uchaguzi  Katika Mapendekezo ya UWT kwenye Sheria ya Vyama Vya Siasatulisemaasilimia fulani ya Ruzuku itumike kuwajengea uwezo wanawake namakundi maalum kuweza kushiriki katika Chaguzi na sasa katika Sheria ya TumeyaUchaguzi tunapendekeza kuwa Tume isimamie matumizi ya fedhafedhazaUchaguzi katika kuimarisha ushiriki wa wanawake na makundi maalum 

MSWAADA WA SHERIA YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI 

Kifungu cha 32  Sheria itamke kuwa Mgombea Kiti cha Rais akiwa wa jinsia mojabasi Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais atakuwa wa jinsia ingine Kifungu cha 50  UWT tunatambua kuwa katika Ubunge tuna asilimia 30% ambayo ipoKikatibahali kadhalia kwa Madiwani Viti Maalum lakini kwa upande wa Serikali zaMitaa hakuna kitu kama hiki  Kwakuwa moja ya malengo ya UWT ni kuchagiza kufikia 50/50 Bungeni na ngazi ya Madiwani ina maana ili kufikia hapo ni lazima Wanawake waende katika nafasi za kugombea Majimbo na Kata  Hivyo basi, ili kuipa meno Tume ya Uchaguzi kusimamia utekelezaji wa usawa wa kijinsia katika chaguzi, Sheria ya Tume ya Uchaguzi iseme piakuwaangalau asilimia 20% ya Wagombea wa Majimbo, Udiwani, Serikali za Mitaana katika Chaguzi za ndani ya Vyama watakuwa Wanawake.

 Kifungu cha 51, kifungu kidogo 1 na Kifungu 63, kifungu kidogo 1  UWT inapendekeza kwamba Sheria ya Uchaguzi wa Rais, WabungenaMadiwani iweke kiwango cha Wanawake na makundi maalum kulipia nusu ya kiwango cha fedha kitakachotakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ili kuwawezesha kujitokeza kugombea kwa wingi zaidi,
 Kifungu cha 60, Kifungu kidogo cha 1  Sheria iongeze kosa kuhusu ukatili wa kijinsia katika orodha yamakosayanayoweza kupelekea mtu kukosa sifa ya kuteuliwa katika Uchaguzi hivyoSheria itamke wazi ikiwa mgombea amethibitika kufanya vitendovyaukatili wa kijinsia ikiwemo unyanyasaji wa kingono na ukatili wa kijinsia mtandaoni na suala hili liwe kwa kipindi chote yaani kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Kifungu cha 112 na Kifungu cha 113  Sheria iweke mfumo wa namna ya kuwapata Wabunge wa Viti Maalum na Madiwani wa Viti Maalum tofauti na hivi sasa ambapo ni CCM pekee ya keyenye utaratibu unaojulikana na hii itasaidia sana kupambana na ukatili wakijinsia kwa wanawake katika siasa ndani ya Vyama Vya Siasa


Mdau, nakuoamba uendelee kusilkiliza kupitia clip hii ya video, Chatanda akisoma mapendekezo hayo...

 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages