LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2024

CCM ARUSHA YAIPA SIKU TATU TARURA KUFUTA ADHA YA UKOSEFU WA KIVUKO

Na Mwandishi Maalum, Arusha

SEKRETARIETI  ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Arusha imetoa siku tatu kwa wakala wa barabara za Mijini na Vijijini(TARURA) wilaya ya Arusha kuanza mara moja ujenzi wa kivuko cha barabara ya Sojema ambacho kimewatesa wananchi wa mtaa huo kwa miaka kumi.

Akizungumza wakati wa ziara ya mtaa kwa mtaa  ya Sekretarieti hiyo ya CCM wilaya ya Arusha ikiongozwa na Katibu wa CCM wilaya ya Arusha Timoth Sanga  amesema halmashauri ya Jiji la Arusha imetenga fedha kwa ajili ya ukarabari wa barabara za ndani ya Jiji ziliharibiwa na mvua pamoja na vivuko hivyo hakuna sababu za TARURA kutojenga kivuko hicho.

“Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Arusha Mhandisi Fadhili Mosses nakupa siku tatu uwe  umewasilisha  mchoro wa ki6vuko cha Sojema ofisini kwangu na Mimi nitashiriki ujenzi huo na kufuatilia kwa karibu ndani ya mwezi mmoja kiwe kimekamilika haiwezekani CCM tupo halafu wanawake wanajifungulia njiani na watoto kushindwa kwenda shule kisa kivuko cha Sojema hii haikubaliki”.

Kwa mujibu wa Sanga haiwezekani wananchi wanakabiliwa na changamoto ya kivuko kwa zaidi ya miaka kumi licha ya kuvunja nyumba zao bila fidia kwa maelekezo ya TARURA halafu kivuko kisijengwe huku ni kuwachonganisha wananchi ya serikali inayoongozwa na CCM”.

“Niwaombe sana wananchi wa kata ya Murieti muendelee kuwa na Imani na CCM kwa sababu ndiyo yenye serikali na sisi tutapokea changamoto zenu na kuilekeza izifanyie kazi kwa wakati kwa sababu tofauti na hivi sasa ambapo mmepewa ahadi ya kivuko kwa muda mrefu bila mafanikio”.

Mhandisi Mosses aliwaahidi wajumbe hao wa Sekretarieti kuwa ndani ya siku tatu atawasilisha mchoro kwao wa kivuko hicho  na kwamba ujenzi wake utaanza mara moja na kukamilika katika kipindi cha mwezi mmoja.

“Ni kweli changamoto hii ni ya muda mrefu na tumeshakuja hapa mara kadha lakini bajeti yetu ilikuwa finyu lakini nimekuja hapa na mkandarasi  kwa kuwa halmashauri ya Jiji imetuhakikishia kuwa fedha za ujenzi zipo tunaahidi kuanza ujenzi mara moja”.

Mkandarasi wa kamapuni ya DCI, Imamu Mvungi anayetakiwa kutekeleza ujenzi wa mradi wa kivuko hicho alisema yuko tayari kuanza kazi na achohitaji kwa sasa ni kupewa mkataba ili kazi hiyo ianze mara moja.

“Katibu maelekezo yote uliyoyatoa hapa nimeyapokea niko tayari kuanza kazi hata sasa hivi iwapo nitakabidhiwa mkata kwa sababu kuna kazi nyingine nyingi za barabara ambazo ninazitekeleza katika halmashauri ya Jiji la Arusha lakini changamoto ni mkataba”.

Awali Diwani wa kata ya Murieti Fracis Mbise alimshukuru katibu Sanga pamoja na wajumbe wa sekretarieti ya wilaya kwa kutaua changamoto hiyo ambayo imewatesa wananchi kwa miaka mingi licha yay eye kwenda ofisi za TARURA mara kwa mara bila mafanikio.

Mwanaisha Ally alisema mwarobaini wa changamoto hiyo kupatikana kwa kuwa kivuko hicho kilikuwa kinadababisha changamoto kubwa ya wanafunzi kushindwa kwenda shule pamoja na wagonjwa hasa kina mama wajawazito.

Katibu wa CCM wilaya ya Arusha Timoth Sanga

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages