LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 28, 2023

MAKONDA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI.

Geita, Tanzania
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi na Uenezi Paul Makonda, amewaomba Viongozi wa Dini nchini, kudumisha ushirikiano na viongozi wa CCM na Serikali na kutoa ushauri kwa viongozi hao utakaowasaidia kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa haki.

Mwenezi Makonda amesema ushauri wa viongozi hao wa dini nchini utawezesha Chama na Serikali kufikia ufanisi unaogusa matumaini ya Watanzania kwenye nyanja mbalimbali hususan katika maendeleo ya Kiuchumi na kijamii.

Mwenezi Makonda ametoa ombi hilo alipokwenda kumsalimia Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, Ofisini kwake, mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, leo Alhamisi, Disemba 28, 2023.

Alienda ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wake wa kwenda kuwaomba ushirikiano, ushauri na miongozo mbalimbali viongozi wa kiroho wa madhehebu ya dini nchini, pamoja na makundi mengine ya kijamii, utakaomsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake.

Katika mazungumzo, Mhashamu Baba Askofu Kassala, pamoja na kumtakia kila la heri, amemhakikishia Mwenezi Makonda kuwa viongozi wa Dini wataendelea kutoa ushirikiano wao katika kuiombea Nchi, kuwashauri Viongozi na kuwapatia miongozo mbalimbali itakayowasaidia kuendelea kuwa watumishi bora wa wananchi, wanapotekeleza majukumu yao ya kuiongoza nchi kwa haki na upendo ili pia kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Aidha, Kwa pamoja wamefanya maombi ya kuliombea Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dk. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuwa na Afya njema na kuendelea kulitumikia Taifa la Tanzania.

Amemuombea Mwenezi Makonda Muumba amjalie kuwa na afya nje, na katika nafasi yake aongoze kwa hekima, busara na maarifa kwa manufaa ya taifa.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda aizungumza na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, Ofisini kwake, mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, leo Alhamisi, Disemba 28, 2023.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, akimbariki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda katika Ibada fupi iliyofanyika katika Kanisa hilo mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, leo Alhamisi, Disemba 28, 2023.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, akimbariki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda katika Ibada fupi iliyofanyika katika Kanisa hilo mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, leo Alhamisi, Disemba 28, 2023.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, akimuinua Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda baada ya kumbariki katika Ibada fupi iliyofanyika katika Kanisa hilo mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, leo Alhamisi, Disemba 28, 2023.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala, akimbariki katika viganja, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda baada ya Ibada fupi iliyofanyika katika Kanisa hilo mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, leo Alhamisi, Disemba 28, 2023.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Paul Makonda akimshukuru
Askofu Katoliki Jimbo la Geita Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala,
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda akizungumza na Watawa nje ya Kanisa hilo kabla ya kuondoka.
Kanisa Katoliki Jimbo la Geita mkoani Geita.

Tazama video: 👇


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages